Matatizo ya kiuchumi yanayoikabili dunia hivi sasa yasiwe sababu ya mataifa tajiri kutotimiza wajibu wao wa ahadi walizotoa kwa nchi zinazoendelea. Huo ni ujumbe aliorejea kuutoa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon alipowasili Busan, Korea ya Kusini Jumanne.