António Guterres

Ukiwaengua raia, demokrasia katu haiwezi kuishi wala kusharimi- Guterres

Leo ni siku ya kimataifa ya demokrasia ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito kwa nchi zote duniani kuimarisha uthibiti wa kidemokrasia, na wananchi wote duniani kuweka ahadi ya kutambua na kulinda haki za binadamu pamoja na kuheshimu utawala wa sheria kama msingi wa demokrasia.

Guterres: Ushirikiano wa Kusini- Kusini unahitaji zaidi sasa kuliko awali

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya ushirikiano wa kusini – kusini UNOSSC imefanya mkutano wake wa ngazi za juu kwa njia ya mtandao siku ya ijumaa (10 septemba 2021) ukilenga kukuza mshikamano "kuunga mkono mustakabali wa ujumuishi, wenye ujasiri na endelevu". 

Miaka 20 ya 9/11 Guterres aomboleza waokoaji waliokufa katika tukio hilo

Ikiwa leo ni kumbukumbu ya miaka 20 shambulio la kigaidi katika majengo makubwa mawili ya biashara mjini New York nchini Marekani,  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ameomboleza waokoaji waliokimbilia ndani ya majengo hayo kuokoa maisha ya watu na wao kupoteza maisha yao baada ya majengo hayo kuporomoka.  

Umoja wa Mataifa waadhimisha miaka 60 ya kifo cha Dag Hammarskjöld

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa hii leo Septemba 09, 2021 limefanya hafla ya kumbukumbu yakuadhimisha miaka 60 ya kifo cha Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Dag Hammarskjöld.

Tumemuomba Guterres asiwasahau watanzania katika nafasi za juu za uongozi: Mulamula 

Waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa wa Tanzania, Balozi Liberata Mulamula amefanya ziara maalum katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani, kuwasilisha ujumbe wa rais wa nchi hiyo Samia Suluhu Hassan.

Tunatakiwa kusherekea utajiri wa dini zetu na sio chuki: Guterres

Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kuwakumbuka waathirika wa vitendo vya vurugu zilizotokana na dini au imani, ulimwengu bado unashuhudia ongezeko la kauli za chuki, kutovumiliana, na hata mashambulio ya mwili kwa watu, vikundi au maeneo, sababu ikiwa ni imani yao ya dini au umuhimu wake.

Tuwasikilize na kupaza sauti kutetea haki za waathirika wa ugaidi: Guterres

Leo tarehe (21 Agosti) ni siku ya kumbukizi na kuwaenzi waathirika wa ugaidi duniani. 
Katika kuadhimisha siku hii, Umoja wa Mataifa unaungana na waathirika wote pamoja na jamii zilizo athirika na kuwapoteza wapendwa wao kutokana na vitendo vya kigaidi

Katibu Mkuu wa UN atoa wito kwa pande zote Afghanistan huku  Baraza la Usalama likitegemewa kukutana Jumatatu hii. 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres anafuatilia hali ilivyo huko Afghanistan akiwa na wasiwasi mkubwa na amewasihi Taliban na wahusika wote wajizuie kwa kiwango cha juu ili kuepusha madhara kwa raia na pia kuhakikisha utoaji wa misaada ya kibinadamu. 

Sasa ni wakati wa kuepusha vita isiyo na ukomo Afghanistan – Guterres

Huu ni wakati wa Afghanistan kuacha mashambulizi, huu ni wakati wa kuanza mazungumzo makini na huu ni wakati wa kuepusha vita vya wenyewe kwa wenyewe visivyokoma, ndivyo ambavyo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametamatisha mkutano wake na waandishi wa habari hi leo jijini New York, Marekani baada ya kurejea tu kutoka likizo.

UN inafuatilia uchaguzi mkuu nchini Zambia

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema anafuatilia kwa karibu uchaguzi mkuu nchini Zambia unaofanyika leo tarehe 12 Agosti 2021.