António Guterres

Maadili yaliyoanzisha Umoja wa Mataifa hayana muda wa kumalizika

Hii leo ni siku ya Umoja wa Mataifa ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema miaka 76 iliyopita, Umoja wa Mataifa uliundwa kama gari la kuleta matumaini kwa ulimwengu uliokuwa unaibuka kutoka kivuli cha mzozo mbaya wa Vita Kuu ya Pili ya dunia.

22 Oktoba 2021

Leo kama ilivyo ada ya Ijumaa tunakuletea mada kwa kina tukimulika siku ya Umoja wa Mataifa inayoadhimishwa tarehe 24 mwezi huu wa Oktoba.

Sauti -
14'4"

Ghasia zikiripotiwa Eswatini, Guterres asihi pande kinzani zijadiliane

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres anafuatilia kwa wasiwasi mkubwa kile kinachoendelea nchini Eswatini, ikiwemo hatua ya hivi karibuni ya kupelekwa kwa wanajeshi katika shule mbalimbali nchini humo.

Tumejenga mfumo wa ulimwengu ambao unaongeza mgawanyiko kati ya mataifa – Uhuru Kenyatta 

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ambaye ndiye ameongoza kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo tarehe 12 Oktoba 2021 kutokana na kwamba nchi yake ndio inakalia kiti cha urais wa Baraza hilo, amesema mizozo mingi ni kutokana na malalamiko yasiyosimamiwa vizuri. 

Kwa Afghanistan, huu ni wakati wa kujenga au kubomoa- Guterres

Janga la kibinadamu likiendelea nchini Afghanistan, hii leo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ameisihi dunia ichukue hatua haraka kwa kuwa muda huu sasa ni wa kujenga au kubomoa kwa taifa hilo la Asia.
 

Jarida 30 Septemba 2021

Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya sekta ya bahari , janga la corona au COVID-19 limethibitisha umuhimu wa bahari na kujitolea kwa mamilioni ya mabaharia wanaofanyakazi katika sekta hiyo amesem

Sauti -
12'14"

UN kusaidia Tanzania kufanikisha Ajenda 2030

Mara baada ya kuhutubia mjadala mkuu wa mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGA76 jijini New York, Marekani, Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania alikuwa na mazungumzo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres.
 

Jarida 20 Septemba 2021

Katika Jarida hii leo Flora Nducha anakuletea mada kwa kina inayo mulika jinsi Umoja wa Mataifa unachagiza mashinani mifumo endelevu ya chakula ikiwa ni kuelekea mkutano wa ngazi ya juu wa umoja huo hapa New York Marekani kuhusu mifumo ya chakula.

Sauti -
13'57"

Ni wakati wa kupiga kelele ya dharura- Guterres

“Ni wakati wa kupiga kengele ya dharura”, amesema Katibu Mkuu wa UN katika mahojiano maalum na Idhaa ya Umoja wa Mataifa siku chache kabla ya kuanza kwa Mjadala wa Juu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Akihojiwa na Assumpta Massoi wa UN News, António Guterres amegusia ushirikiano wa kimataifa, harakati za utoaji wa chanjo dhidi ya COVID-19 duniani, mabadiliko ya tabianchi, usawa wa jinsia, viijana, amani na usalama barani Afrika na duniani kwa ujumla.

Ukiwaengua raia, demokrasia katu haiwezi kuishi wala kusharimi- Guterres

Leo ni siku ya kimataifa ya demokrasia ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito kwa nchi zote duniani kuimarisha uthibiti wa kidemokrasia, na wananchi wote duniani kuweka ahadi ya kutambua na kulinda haki za binadamu pamoja na kuheshimu utawala wa sheria kama msingi wa demokrasia.