António Guterres

Watekelezaji wa mashambulizi ya kigaidi Nigeria wawajibishwe:Guterres:

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelaani mashambulizi ya kigaidi  ya mara kwa mara yanayofanywa na makundi mengine yenye itikadi kali Kaskazini mwa Nigeria na kusababisha vifo na majeruhi miongoni mwa raia, vikosi vya usalama na kuvuruga utaratibu wa maisha ya kawaida.

Shambulio Afghanistan ni ukiukwaji wa sheria za kimataifa za haki:UN

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelaani vikali shambulio la leo nchini Afghanistan lililowalenga watu waliokusanyika kusheherekea siku muhimu ya kidini.

Zama za kufumbia macho ukatili wa kingono zimepita- Guterres

Suala la amani na usalama barani Afrika leo tena limepatiwa kipaumbele katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambapo wajumbe wamejikita zaidi katika kuangazia operesheni za ulinzi wa amani barani humo.

Ajabu mtu kuteswa kwa sababu ya kuwa na dini tofauti na wenzake- Guterres

Kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa hii leo kumefanyika mkutano wa 8 wa jukwaa la ustaarabu la Umoja wa Mataifa ambapo Katibu Mkuu Antonio Guterres ameelezea kustaajabu kwake jinsi tofauti ya imani ya kidini na tamaduni vinavyoendelea kuwa chanzo cha mauaji na mateso kwa baadhi ya wakazi wa dunia.

Maendeleo ya kweli yatapatikana wanawake na wasichana wakiwa huru- Guterres

Ukatili dhidi  ya wanawake na wasichana ni janga la kimataifa, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres wakati akihutubia tukio maalum la siku ya kimataifa ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake lililofanyika kwenye makao makuu ya umoja  huo jijini New York, Marekani hii leo.

Walinda amani saba wa UN wauawa DRC: Wanatoka Malawi na Tanzania

Walinda amani 7 wa Umoja wa Mataifa wameuawa huko Beni, jimbo la Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.

Kuondolewa kwa vikwazo dhidi  ya Eritrea kutachagiza ujenzi wa amani- Guterres

Kufuatia hatua ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuondoa vikwazo dhidi ya Eritrea, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, amesema anafuatia kwa karibu maendeleo ya sasa huko Pembe ya Afrika akisema ni matumaini yake kuwa kuondolewa kwa vikwazo hivyo kutachangia katika kusongesha juhudi za amani kwenye eneo hilo.

Guterres asema wahusisheni wadau kutoka kila nyanja ya Intaneti

Akihutubia mkutano wa jukwaa la usimamizi wa intaneti,IGF,unaofanyika hii leo mjini Paris Ufaransa,  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa

Sauti -
2'11"

Guterres aelezea mshikamano wake na Marekani kufuatia moto jimboni California

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameelezea kusikitishwa kwake kufuatia taarifa za vifo na uharibifu mkubwa kutokana na moto wa nyika unaoendelea kukumba jimbo la California nchini Marekani.

Husisheni wadau kutoka kila nyanja mnapojadili kuhusu teknolojia ya intaneti-Guterres

Akihutubia mkutano wa jukwaa la usimamizi wa intaneti,IGF,unaofanyika hii leo mjini Paris Ufaransa,  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema, katika miaka 13 tangu mkutano wa kimataifa uliofanyika Tunisia mwaka 2005, dunia ya kidijitali imebadilika kwa kasi, fursa mpya zimefunguka na hivyo masuluhisho ya kidijitali yanabadili maisha ya watu na kwamba yanaweza kusongesha mbele kazi ya kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs.