António Guterres

Mauaji ya Gaza leo lazima yachunguzwe: Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametoa wito wa kufanyika uchunguzi huru na wa wazi dhidi ya machafuko yaliyozuka leo Ijumaa kwenye uzio wa Gaza kati ya Wapalestina waliokuwa wakishiriki maandamano na vikosi vya ulinzi vya Israel na kusababisha vifo vya watu 15 na wengine wengi kujeruhiwa.

Tuhakikishe wanawake na wasichana wenye usonji hawaachwi na treni ya 2030: Guterres

Katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya uelimishaji kuhusu usonji, ambayo kila mwaka hua Aprili pili, Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa amesisitiza kusimamia haki ya watu wenye usonji na kupazia sauti ubaguzi dhidi yao.

Mvutano wa Marekani na Urusi unanitia wasiwasi

Mvutano kati ya Urusi na Marekani uliosababisha hata pande mbili hizo kuchukua hatua za kufukuziana maafisa wao wa kibalozi unanitia wasiwasi mkubwa.

Sauti -
1'20"

Ushahidi gani zaidi wahitajika kuamini mabadiliko ya tabianchi yapo?

Watu 900,00 barani Afrika wamekimbia makazi yao kutokana na ukame. Nchi za kusini mwa Asia zimeshuhudia mafuriko makubwa yaliyoathiri awtu milioni 41. Gharama za kiuchumi kutokana na majanga yatokanayo na mabadiliko ya tabianchi ni dola bilioni 320. Hii imevunja rekodi!

Sauti -
1'47"

Je vita baridi vyanukia upya?

Chonde chonde vita baridi si kwa wakati huu kwani mwelekeo huu si mzuri na unatia hofu. 

Kengele ngapi zigongwe tudhibiti mabadiliko ya tabianchi? Guterres

Mkutano na waandishi wa habari, Guterres amulika zaidi mabadiliko ya tabianchi na hatua anazoamini kuwa zinapaswa kuchukuliwa. Azungumzia pia matarajio yake kuhusu kinachoendelea rasi ya Korea na mvutano kati ya Urusi na mataifa mengine duniani.

Twashambuliwa lakini hatukati tamaa- Guterres

Operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa wakati huu zinafanya kazi katika mazingira magumu tena yenye hatari kubwa.

Sauti -
1'53"

Walinda amani wanajitoa kimasomaso- Guterres

Ulinzi wa amani unakumbwa na changamoto kila uchao ambapo walinda amani wanashambuliwa na kuuawa, lakini bado hawakati tamaa kwani lengo kuu ni amani na  usalama duniani.

Saudi yaahidi dola milioni 930 kuwanusuru Wayemen:

Ufalme wa Saudia umeahidi kutoa dola milioni 930 kwa ajili ya mfuko wa usaidizi wa kibinadamu kwa watu wa Yemen.

Tuzidishe juhudi kulinda watumishi wa UN-Guterres

Hebu tuimarishe azma yetu ya pamoja na njia za kuwalinda wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wakati wakifanya kazi zao bila kuchoka kwa ajili ya amani,maendeleo endelevu na vilevile haki za watu wote, amesema

Sauti -
1'30"