Skip to main content

Chuja:

Antoni Guterres

04 AGOSTI 2023

Hii leo jaridani tunaangazia haki za binadamu na Akili Mnemba au ‘Artificial Intelligence’.  Makala tunakupeleka nchini Brazil na mashinani tutasikia ujumbe wa kijana kutoka Tanzania, salía papo hapo!  

Sauti
11'25"

06 APRILI 2023

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo tunaangazia afya ya uzazi na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya afya ya uzazi salama kwa wanawake kutoka hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Dk. Elieza Chibwe akizungumzia juu ya kukoma kwa hedhi kwa wanawake anasema “Ukihisi dalili za menopause mapema nenda hospitali.” Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo salamu za sikukuu za Pasaka na Eid El Fitr kutoka kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ombi la UNICEF la msaada kwa watoto waathirika wa matetemeko ya ardhi huko mashariki ya kati, na haki za watu wa jamii asili.

Sauti
13'2"
UNAMI/Sarmad al-Safy

Katibu Mkuu Guterres ziarani nchini Iraq

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amefanya ziara nchini Iraq lengo likiwa ni kusisitiza mshikamano na kuunga mkono juhudu za nchi za kuleta amani ,haki za binadamu na maendeleo endelevu.

Ziara ya mwisho ya Katibu Mkuu Guterres nchini Iraq ilikuwa miaka sita iliyopita, na alipofika Baghdad alipokelewa na Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya nje Fued Hussein ambapo walifanya mkutano wa pamoja na waandishi wa habari.

Sauti
2'6"