Americas

Wataalamu wa UM waitaka Marekani kushughulikia ukatili wa polisi na dhuluma za ubaguzi wa rangi

Alama za utumwa zinasalia kuwa changamoto kubwa nchini Marekani kwa kuwa kumekuwa hakuna ahadi ya kweli kutambua na kuwalipa fidia watu wenye asili ya Afrika, limesema leo jopo la wataalamu wa Umoja mwishoni mwa ziara yao ya pili rasmi nchini humo.

Sauti -

Wataalamu wa UM waitaka Marekani kushughulikia ukatili wa polisi na dhuluma za ubaguzi wa rangi

Baraza la usalama latiwa mashaka na kuahirishwa duru ya mwisho ya uchaguzi Haiti

Wajumbe wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa wamelezea wasiwasi wao kuhusu hali inayoelekea kuahirishwa moja kwa moja duru ya mwisho ya uchaguzi nchini Haiti, ambao awali ulikuwa ufanyike Disemba 27, kisha ukaahirishwa kwa mara ya pili hadi Januari 24 na hadi sasa hauajafanyika.

Sauti -

Baraza la usalama latiwa mashaka na kuahirishwa duru ya mwisho ya uchaguzi Haiti

Mkataba wa Paris kutoka COP21 umeanza kuzaa matunda:Pasztor

Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya mabadiliko ya tabianchi ambaye amemaliza muda wake, Janos Pazstor, amesema mkataba wa mabadiliko ya tabianchi uliopitishwa mwaka jana Paris, Ufaransa umeanza kuzaa matunda.

Sauti -

Mkataba wa Paris kutoka COP21 umeanza kuzaa matunda:Pasztor

UNEP, ZAYED kutenegeza kitabu kuhusu uchumi rafiki kwa mazingira

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa mazingira UNEP na taasisi ya kimataifa ya mazingira iitwayo Zayed leo wametia saini makubaliano ya kuzalisha kitabu cha kiada

Sauti -

UNEP, ZAYED kutenegeza kitabu kuhusu uchumi rafiki kwa mazingira

Kunyonyesha kunapunguza vifo kwa watoto na saratani kwa kina mama: UNICEF

Mfululizo wa nyaraka zilizochapishwa na jarida la kitabibu la The Lancet la Uingereza zinatoa ushahidi kwamba kuimarisha mazoea ya kunyonyesha kunaweza kuokoa maisha ya watoto zaidi ya 820,000 kwa mwaka, huku 9 kati 10 wakiwa ni watoto wachanga wa umri wa chini ya miezi sita.

Sauti -

Kunyonyesha kunapunguza vifo kwa watoto na saratani kwa kina mama: UNICEF