Americas

Ukatili dhidi ya wanawake unatisha: Cameroon matiti ya wasichana yapigwa pasi kuondoa mvuto

Mkutano wa siku mbili ulioandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake, UN-WOMEN mjini New York, Marekani umemalizika kwa mataifa 12 kuitikia wito wa shirika hilo wa kuzitaka nchi dunia kuongeza juhudi za kutokomeza vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake.

Sauti -

Ukatili dhidi ya wanawake unatisha: Cameroon matiti ya wasichana yapigwa pasi kuondoa mvuto

Uandikwaji wa rasimu kuhusu mageuzi ya mawasiliano wakamilika: UM

Wajumbe zaidi ya 160 waliokuwa wanakutana huko Doha, wamekamilisha hatua ya kwanza muhimu ya uandikaji wa rasimu ambayo inakusudia kutumika kwa ajili ya kuyafanyia marekebisho miongozo ya mawasiliano duniani.

Sauti -

Uandikwaji wa rasimu kuhusu mageuzi ya mawasiliano wakamilika: UM

UM wahitaji dola Bilioni 8.5 kwa ajili ya misaada ya kibinadamu mwaka 2013

Umoja wa Mataifa umetangaza ombi la dola Bilioni 8.5 kwa ajili ya operesheni zake za misaada ya kibinadamu kwa mwaka 2013. Fedha hizo zinalenga kuwahudumia watu Milioni 51 kutoka nchi 16 duniani ambao wanahitaji misaada ya kibinadamu.

Sauti -

UM wahitaji dola Bilioni 8.5 kwa ajili ya misaada ya kibinadamu mwaka 2013

Idadi ya watalii kwa mwaka 2012 duniani kote leo yafikia Bilioni Moja

Idadi ya watalii waliotembelea dunia hii leo imetimia Bilioni Moja na kuweka rekodi mpya kwenye utalii wa kimataifa sekta inayochangia nafasi moja kwa kila ajira 12 duniani.

Sauti -

Idadi ya watalii kwa mwaka 2012 duniani kote leo yafikia Bilioni Moja

Licha ya mafanikio safari bado ni ndefu kufikia usawa wa kijinsia: WU

Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya uchumi na kijamii, Wu Hongbo amesema kazi zaidi inahitajika kufanyika kufikia usawa wa kijinsia licha ya hatua zilizofikiwa kutokana na utekelezaji wa malengo ya maendeleo ya milenia.

Sauti -