Americas

Maisha ni magumu kwa watoto duniani, kwa sababu ya ukosefu wa ulinzi unaofaa, inasema ripoti ya UNICEF

Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) limetangaza ripoti mpya, siku ya leo, kutokea mjini Tokyo, Ujapani kuhusu hifadhi ya watoto kimataifa.

BU lasisitiza wanawake washirikishwe kikamilifu katika ujenzi wa amani

Baraza la Usalama (BU) leo limefanyisha mkutano wa hadhara, wa siku nzima, ambao wawakilishi wa kimataifa 55 walizungumzia kuhusu suala la ‘Wanawake, Amani na Usalama\'.

Siku Kuu ya Kuwahishimu Walimu Duniani

Tarehe ya leo, tarehe 05 Oktoba, huadhimishwa na UM kuwa ni ‘Siku ya Walimu Duniani\'. Kwa mujibu wa taarifa ya Kitengo cha Taasisi ya Takwimu ya Shirika la UM juu ya Ilimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), kuanzia 2007 hadi 2015 kulihitajika kuajiriwa walimu milioni 10.3 kwa walimwengu kuweza kukamilisha, kwa wakati, lengo la kuwapatia ilimu ya msingi watoto wote wa kiume na wa kike wanaostahiki kuhudumiwa kadhia hiyo.

Pengo la ustawi laendelea kupanuka baina ya mataifa tajiri na maskini, imebainisha kiashirio cha HDI

Kwenye taarifa kuhusu Kiashirio cha Matokeo ya Utafiti juu ya Maendeleo ya Wanadamu, ambacho hujulikana kama Kiashirio cha HDI, iliowakilishwa mapema wiki hii, iliripotiwa kwamba licha ya kuwa nchi nyingi wanachama zilionyesha kuwa na maendeleo ya kiuchumi na kijamii mnamo miaka 25 iliopita, hata hivyo, pengo la tofauti kuhusu ustawi wa jumla, na hali njema baina ya nchi tajiri na nchi maskini, linaendelea kupanuka.

Hapa na Pale

Mapema Ijumaa, KM BanKi-moon alikutana mjini Stockholm na Spika wa Bunge pamoja na wawakilishi wa vyama vya kisiasa. Baada ya hapo KM alikuwa na mazungumzo na wawakilishi wa mashirika yasio ya kiserikali ya Uswidini. Kufuatia hapo KM alielekea Copenhagen, ambapo alitarajiwa kukutana kwa mazumgumzo na Waziri Mkuu wa Denmark, Lars Lokke Rasmussen, na vile vile Jacques Rogge, Raisi wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC). Ijumamosi KM atahutubia Baraza Kuu la Olimpiki ambapo aantazamiwa kujadilia ajenda ya Kamati ya IOC kuhusu Hifadhi ya Mazingira kwenye Shughuli za Michezo.

Siku ya Kimataifa ya Kutotumia Nguvu wala Mabavu

Hii leo UM unaadhimisha Siku ya Kimataifa Dhidi ya Matumizi ya Nguvu. Risala ya KM juu ya siku hii imetoa mwito maalumu unaoutaka umma wote wa kimataifa kuiadhimisha siku hiyo kwa kukumbushana urithi wa kimaadili wa Mahatma Gandhi ambaye aliwahimiza walimwengu kutatua mifarakano yao kwa taratibu za amani, zisiotumia nguvu, mabavu wala fujo.

Vietnam yachukua madaraka ya kuongoza Baraza la Usalama kwa Oktoba

Kuanzia siku ya leo, Vietnam imekabidhiwa Uraisi wa Baraza la Usalama kwa mwezi Oktoba. Balozi wa Kudumu wa Vietnam katika UM, Le Luong Minh, sasa hivi anashauriana na wajumbe wa Baraza la Usalama juu ya ratiba ya mwezi huu kuhusu shughuli zao.

UM inaadhimisha Siku Kuu ya Kuwahishimu Watu Waliozeeka

Tarehe ya leo, Oktoba 01, inaadhimishwa na UM kuwa ni Siku ya Kimataifa kwa Watu Waliozeeka. Kwenye risala aliotuma KM kuihishimu siku hii, alitoa mwito maalumu uitakayo walimwengu kukomesha tabia ya kubagua wazee wenye umri mkubwa.

Ufufuaji uchumi wapamba moto duniani, kuripoti IMF

Ripoti ya karibuni ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) juu ya hali ya uchumi duniani, imeeleza kwamba kwenye soko la kimataifa, kumeanza kushuhudiwa dalili za kutia moyo, za kukua kwa uchumi, baada ya serikali kadha kuingilia kati masoko yao ya kifedha, kwa kuchangisha msaada wa kufufua shughuli zao na kupunguza hali ya wasiwasi iliojiri, ili kukidhi bora mahitaji ya umma.