Americas

Udhalilishaji dhidi ya wanawake bado waendelezwa kwenye maeneo ya mapigano, atahadharisha ofisa wa kamati ya CEDAW

Naéla Gabr, mwenyekiti wa kamati inayosimamia utekelezaji wa Mkataba wa UM Kuondosha Aina Zote za Ubaguzi Dhidi ya Wanawake (CEDAW) Ijumatatu alipohutubia Baraza Kuu aliwaeleza wajumbe wa kimataifa kwamba vitendo vya unyanyasaji na udhalilishaji katili wa wanawake walionaswa kwenye mazingira ya mapigano bado umeselelea duniani,

KM asema Mpango wa Utendaji wa Cairo juu ya uzazi bora bado haujatekelezwa kama inavyostahiki

Baraza Kuu la UM limeadhimisha leo hii miaka 15 tangu Mkutano wa Kimataifa juu ya Udhibiti wa Idadi ya Watu na Maendeleo uliofanyika Cairo katika 1994 kupitisha Mradi wa Utendaji wa Cairo.

Utafiti wa ILO/WFP umethibitisha ajira isio rasmi huzinyima nchi maskini natija za biashara ya soko la kimataifa

Utafiti ulioendelezwa bia karibuni na Shirika la UM juu ya Haki za Wafanyakazi (ILO) na Shirika la Biashara Duniani (WTO) umegundua kuwa ajira kubwa isio rasmi hukutikana katika nchi zinazoendelea,

Ripoti ya mwaka ya UNICEF juu ya hifadhi ya watoto imesisitiza bidii zaidi zahitajika kuwalinda watoto dhidi ya udhalilishaji

Ripoti ya mwaka ya UNICEF kuhusu hifadhi ya watoto kimataifa imeeleza kwamba licha ya kuwa karibuni kulipatikana maendeleo kwenye suala hilo, watoto bado wanaendelea kudhalilishwa na kukabiliwa na vitendo karaha kadha wa kadha dhidi yao.

KM Ban Ki-moon ampongeza Raisi Obama kwa ushindi wa Tunzo ya Amani ya Nobel kwa 2009

Leo asubuhi KM Ban Ki-moon amekaribisha kidhati tangazo la kuwa Raisi Barack Obama wa Marekani amezawadiwa Tunzo ya Amani ya Nobel kwa 2009.

Maambukizi ya H1N1 kwenye kizio cha kusini cha dunia yameteremka,WHO imeripoti

Shirika la Afya Duniani (WHO) limeripoti maambukizi makubwa zaidi ya homa ya mafua ya A/H1N1 yanasajiliwa kutukia sasa hivi kwenye kizio cha kaskazini chaa dunia, kwa sababu eneo hili linaingia kwenye majira ya homa ya mafua kwa sasa.

Mazungumzo ya Bangkok yamezaa matokeo yenye uwazi juu ya usanifu unaohitajika kujikinga na madhara ya kimazingira

Kikao cha majadiliano ya mwisho mwisho, kilichofanyika Bangkok, Thailand kwa muda wa wiki mbili kimekamilisha mazungumzo yake leo Ijumaa, miezi miwili kabla ya Mkutano wa kihistoria juu ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa utakaofanyika mwezi Disemba kwenye mji wa Copenhagen, Denmark.

Mkuu wa UNFCC anasema mchango ziada wa viongozi wa kimataifa unatakiwa kukamilisha Makubaliano ya Copenhagen

Yvo de Boer, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya UM kuhusu Mkataba wa Kudhibiti Mabadiliko ya Hali ya Hewa (UNFCCC) ameripoti kupatikana maendeleo ya kutia moyo, kwenye mazungumzo ya matayarisho ya waraka wa kuzingatiwa kwenye Mkutano wa Copenhagen juu ya mabadiliko ya hali ya hewa.

UM watahadharisha, uwekezaji mkubwa wa kilimo unatakikana 2050 kutosheleza mahitaji ya chakula kwa watu bilioni 9.1

Wataalamu wa UM wameripoti kwenye makala ya majadiliano, iliochapishwa rasmi siku ya leo na Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) kwamba kunahitajika kufanyika uwekezaji mkubwa wa katika sekta ya kilimo, kuhudumia chakula umma wa kimataifa kwa siku za baadaye, umma ambao ilisema unaendelea kuongezeka kwa kasi kuu.

Mkuu wa Benki Kuu ya Dunia ameahidi mabadiliko yanayofaa kukabili mizozo mipya ulimwenguni

Mkutano wa mwaka wa Kundi la Benki Kuu ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) unaofanyika wiki hii kwenye mji wa Istanbul, Uturuki unazingatia mizozo ya kiuchumi na kifedha iliokabili ulimwengu katika kipindi cha hivi sasa.