Americas

FAO kuanzisha mashauriano ya kubuni miongozo halisi juu ya umiliki bora wa mali ya asili

Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) limeanzisha mashauriano ya awali kihistoria, na wadau kadha wa kimataifa kusailia miongozo inayohitajika kimataifa juu ya udhibiti bora wa umiliki wa ardhi na rasilmali nyengine za kimaumbile, mathalan, maji safi, rasilmali ya uvuvi na mali ya asili ya misitu.

Ripoti ya WHO imethibitisha 'mamilioni ya vifo vya mapema huzuilika kukiimarishwa afya ya msingi'

Ripoti mpya iliochapishwa siku ya leo na Shirika la Afya Duniani (WHO) ilieleza kwamba mamilioni ya vifo vya kabla ya wakati duniani vinaweza kuzuiliwa, kwa kushughulikia mapema matatizo ya aina tano yenye kuhusu afya.

"Wakati umewadia, kuharakisha utekelezaji wa lengo la tano la MDGs, na kupunguza vifo vya uzazi", asema Mkuu wa UNFPA

Ijumatatu kwenye mji wa Addis Ababa, Ethiopia, kulifanyika Mkutano wa Wadhifa wa Juu kuzingatia maendeleo katika utekelezaji wa suala la tano la Malengo ya Maendeleo ya Milenia ya kupunguza umaskini na ufukara katika mataifa yanayoendelea.

Makampuni ya bima yajiunga na UM kudhibiti 'uchumi wa kijani'

Kampuni za kimataifa za bima, zinazodhibiti rasilmali inayogharamiwa matrilioni ya dola, zimejiunga na wataalamu mashuhuri wa kimataifa kwenye uchunguzi, wenye kuungwa mkono na UM, wa kuhakikisha viwanda vinatumia utaratibu unaosarifika na usiochafua mazingira.

Maelfu ya waliong'olewa mastakimu Kivu Kaskazini waanza kurejea makwao, imetangaza OCHA

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imeeleza kwamba katika miezi miwili iliopita, inakadiria watu 110,000 waliong\'olewa makazi na mapigano waliweza kurejea makwao katika jimbo la Kivu Kaskazini la JKK.

Tarehe 17 Oktoba inaadhimishwa na UM kuwa ni Siku ya Kimataifa Kuufyeka Umaskini

Mnamo Ijumamosi, tarehe 17 Oktoba, UM utaadhimisha Siku ya Kimataifa Kufyeka Umaskini.

Siku ya Chakula Duniani

Siku ya leo inaadhmishwa na UM kama ni Siku ya Chakula Duniani. Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) watu bilioni moja ziada wanasumbuliwa na njaa sugu ulimwenguni kwa sasa, na hawana uwezo wa kupata chakula.

UNICEF/WHO zimeanzsiha mradi wa kuzuia vifo vya watoto wachanga vinavyosababishwa na kuharisha

Kadhalika, Shirika la UNICEF na Shirika la Afya Duniani (WHO) yameripotiwa kuanzisha mradi mpya wa pamoja, wenye makusudio ya kukinga na kuwatibu watoto na maradhi ya kuharisha - ikiwa ni ugonjwa wa pili wenye kusababisha vifo kwa wingi zaidi miongoni mwa watoto wachanga katika nchi zenye hali duni ya uchumi.

Siku ya Kimataifa Kupunguza Maafa

Tarehe 14 Oktoba huadhimishwa na UM, kila mwaka, kuwa ni Siku ya Kimataifa Kupunguza Maafa (ISDR). Kampeni ya mwaka huu ya kuihishimu siku hiyo inalenga shughuli na taadhima zake zaidi kwenye juhudi za "kuzikinga hospitali na madhara ya maafa ya kimaumbile".

FAO/WFP zahadharisha, mizozo ya uchumi huifanya hali dhaifu ya chakula duniani kuwa mbaya zaidi

Ripoti ya pamoja ya mashirika mawili ya UM yanayohusika na miradi ya chakula na kilimo, yaani FAO na WFP, iliotolewa leo Ijumatano, imeeleza kwamba mzozo wa uchumi uliopamba ulimwenguni kwa sasa ndio uliopalilia tatizo la njaa duniani, kwa kiwango cha hali ya juu kabisa cha kihistoria, ambacho hakijawahi kushuhudiwa tangu 1970.