Hali ya uchumi wa dunia inatazamia kukua kwa wastani mwaka ujao, lakini pia nchi za Ulaya zitakabiliwa na changamoto ya ulipaji madeni ili kudhihirisha ukuaji wa uchumi huo.
Watu 2700 wamefariki dunia kwa kipundupindu nchini Haiti kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA.
Wataalamu wa Umoja wa Mataifa wanaohusika na masuala ya majanga wameongeza nguvu kusaidia shughuli za uimarishaji hali ya maisha kwa mamia ya wananchi wa Colombia ambao wameathiriwa vibaya na mafuriko.
Umoja wa Mataifa umezindua mchezo wa video kwa kutumia wavuti kwa lengo la kuwapa vijana taarifa muhimu kuhusu kuzuia maambukizi ya HIV, huku ukiwaelimisha, kuwaburudisha na kuchagiza tabia njema zinazojali afya zao.
Wakati kikao cha 65 cha baraza kuu la Umoja wa Mataifa kikikunja jamvi, rais wa baraza hilo Joseph Deiss amepongeza mkutano huo ambao amesema ulifungua njia ya kuongeza kasi ya kufikia malengo ya maendeleo ya milenia ya Umoja wa Mataifa na kuondokana na umasikini na maradhi yanayoisumbua dunia.
Ripoti mpya iliyotolewa leo na Umoja wa Mataifa inaonyesha kwamba usafirishaji nje wa bidhaa katika Asia na Pacific unakuwa huku viwango vya uchumi vikiongezeka kwa tarakimu mbili kwa mwaka huu wa 2010.
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amekaribisha kura ya bunge la Marekani ya kuunga mkono kuidhinishwa kwa mkataba wa kupunguza zana za nyuklia uliotiwa sahihi mapema mwaka huu kati ya viongoiz wa Urusi na Marekani.
Mkataba muhimu wa kufuatilia kupotea kiholela au kwa lazima kwa watu unaanza kutekelezwa leo huku wataalamu wa Umoja wa Mataifa wenye jukumu la kuzisaidia familia kujua hatma ya wapi waliko jamaa zao waliopotea, wameyataka mataifa yote kuhakikisha wanakomesha uhalifu huo kwa kuwafikisha wahusika kwenye vyombo vya sheria.