Americas

UM unaadhimisha Siku ya Haki za Binadamu

Tarehe ya leo, 10 Disemba (2009) inaadhimishwa na UM kuwa ni Siku ya Haki za Binadamu. Kwenye risala ya KM juu ya taadhima za siku hii, alihadharisha kwamba hakuna hata taifa moja duniani liliosalimika hivi sasa na tatizo la ubaguzi, tatizo linaloendelea kujiwasilisha kwenye mifumo na miundo aina kwa aina ya kijamii.

Kiashirio cha awali kupima uchafuzi wa gesi za kaboni kimewakilishwa Copenhagen

Shirika la Kimataifa juu ya Usimamizi wa Fedha (IFC), likiwa miongoni mwa taasisi za Kundi la Benki Kuu ya Dunia, likijumuika na Kampuni ya Kimarekani ya Standard & Poor, ambayo hushughulikia ugunduzi wa viashirio vya uwekezaji wa kimataifa, wamebuni kiashirio cha kwanza duniani chenye kupima mabaki ya gesi ya kaboni kwenye masoko ya mataifa yanayoanza kuibuka kiuchumi,

Ripoti fupi kuhusu matukio ya Mkutano Mkuu wa Copenhagen

KM Ban Ki-moon amenakiliwa akifuatilia, kwa ukaribu zaidi, hekaheka na harakati za kijumla kwenye Mkutano Mkuu wa UM juu ya Mabadiliko ya Hali ya hewa, wakati majadiliano yakipamba na kuendelea miongoni mwa wajumbe wa kimataifa.

Wawakilishi wa G-77 waamini kuna rasilmali za kutosha ulimwenguni kukomesha madhara ya mabadiliko ya hali ya hewa

Wawakilishi wa Mataifa wanachama wa Kundi la G-77 na Uchina, wamesisitiza kwenye kauli kadha walizowasilisha kwenye majadiliano ya Copenhagen ya kuwa umma wa kimataifa, kwa ujumla, katika karne ya ishirini na moja, umebarikiwa rasilmali ya kutosha kushughughulikia, kwa mafanikio, matatizo

Ripoti ya FAO yanonyesha bei za chakula zimeanza kupanda tena kwenye soko la kimataifa

Shirika la Chakula na Kilimo (FAO) limehadharisha kwenye ripoti iliochapishwa Ijumatano kwamba bei za juu za chakula, zimeanza kupanda tena katika dunia.

KM awaambia wajumbe wa Mkutano juu ya Mfuko wa CERF "twahitajia misaada zaidi kukabili athari za gesi chafuzi"

Asubuhi kwenye Makao Makuu, kulifanyika kikao maalumu kuzingatia shughuli za ile Taasisi ya Mfuko wa UM juu ya Maafa ya Dharura au Mfuko wa CERF.

Hatua ziada zatakikana dhidi ya matumizi ya tumbaku duniani, inahimiza WHO

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza ripoti mpya inayoeleza kwamba licha ya kuwa idadi kubwa ya umma wa kimataifa huhifadhiwa na zile sheria za kupiga marufuku uvutaji sigara kwenye mazingira ya umma, hasa katika 2008, juu ya hayo tumearifiwa kwamba bado tutahitajia kuchukua hatua ziada za dharura, za kuwalinda watu na maradhi pamoja na vifo vinavyoletwa na athari za moshi wa sigara.

Wataalamu wa kimatafia wanajiandaa kubuni viashirio vipya juu ya mifumko ya ukame duniani

Kuhusu athari za mabadiliko ya hali ya hewa zilizoshuhudiwa kutukia ulimwenguni mnamo miaka ya karibuni, Shirika la UM juu ya Utabiri wa Hali ya Hewa Duniani, (WMO), limebashiria kutatukia muongezeko mkubwa wa marudio ya ukame mkali, katika sehemu mbalimbali za dunia katika miaka ijayo.

Waraka wa siri uliofichuliwa Copenhagen waonyesha mgawanyo wa matarajio kati ya nchi tajiri na zile zenye maendeleo haba

Majadiliano ya Mkutano wa UM juu ya taratibu za kudhibiti bora athari za mabadiliko ya hali ya hewa ulimwenguni, Ijumanne yalikabiliwa na mtafaruku na vurugu lisiotarajiwa, baada mataifa yanayoendelea kuonyesha ghadhabu kubwa juu ya waraka wa siri uliofichuliwa na vyombo vya habari,

Mradi wa DOTS wafanikiwa kutibu TB watu milioni 36

Katika miaka 15 iliopita, watu milioni 36 wanaripotiwa walitibiwa, kwa mafanikio, maradhi ya kifua kikuu, au TB, ulimwenguni, kwa kutumia utaratibu mkali wa kuhudumia afya bora uliotayarishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO).