Americas

Mkutano wa WCC unazingatia utaratibu mpya wa kueneza taarifa za hali ya hewa kote duniani

Mkutano Mkuu wa Dunia juu ya Hali ya Hewa (WCC-3) umefunguliwa rasmi Geneva Ijumatatu ya leo, ambapo wataalamu na wanasiasa kutoka sehemu mbalimbali za ulimwengu, wanakutana kwa mashauriano ya kuhakikisha umma wa kimataifa huwa unapatiwa uwezo wa kutabiri hali ya hewa pamoja na taarifa nyengine kama hizo, ili kukabiliana vyema na taathira za mabadiliko ya hali ya hewa.

Taarifa juu ya hali ya maambukizi ya A/H1N1 katika dunia

Shirika la Afya Duniani (WHO) kwenye taarifa ya wiki kuhusu hali ya maambukizo ya homa ya mafua ya A/H1N1 llimeeleza ya kwamba katika nchi za kizio cha kusini ya dunia, ikijumlisha Chile, Argentina, New Zealand na Australia maambukizo ya maradhi yameshapita kilele na hivi sasa yameselelea kwenye kigezo wastani, wakati mataifa ya Afrika Kusini na Bolivia yanaendelea kukabiliwa na ongezeko la homa ya mafua.

Siku 100 zimesalia kabla ya Mkutano wa COP-15 kudhibiti taathira za mabadiliko ya hali ya hewa

UM umetoa mwito maalumu wenye kuwataka mamilioni ya umma wa kimataifa kutia sahihi zao, kwenye mtandao, ili kuidhinisha lile ombi la kuzihimiza serikali wanachama Kukamilisha Makubaliano juu ya waraka wa Mkutano wa COP-15, yaani ule Mkutano Mkuu utakaofanyika mwezi Disemba katika mji wa Copenhagen, Denmark kuzingatia mkataba mpya wa udhibiti bora wa mabadiliko ya hali ya hewa ulimwenguni.

Wajumbe wa Mkutano wa Kupunguza Silaha wajitahidi kufikia mapatano kwenye mradi wa kazi

Alkhamisi, wajumbe wanaohudhuria Mkutano wa Kupunguza Silaha Duniani, unaofanyika Geneva kwa hivi sasa, bado wanaendelea na juhudi za kusuluhisha mvutano juu ya mradi wa kufanya kazi wa kikao hicho.

Mabatamzinga wa Chile wakutikana na virusi vya H1N1

Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) limetoa taarifa yenye kueleza wafugaji kuku na ndege ulimwenguni wameingiwa wasiwasi mkuu baada ya kugunduliwa homa ya mafua ya A/H1N1 miongoni mwa mabatamzinga wa katika taifa la Amerika Kusini la Chile.

Mwanasheria wa Afrika Kusini ameteuliwa kutetea haki za wanawake waathirika wa matumizi ya nguvu

Taarifa iliotolewa na Ofisi ya Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu (OHCHR) imeleza kwamba wakili kutoka Afrika Kusini, Rashida Manjoo, ameanza rasmi kazi ya Mkariri (Mtetezi) Maalumu mpya wa UM atakayehusika na huduma za kupinga matumizi ya nguvu dhidi ya wanawake, na kuendeleza kampeni za kudhibiti sababu na taathira za udhalilishaji wa kijinsiya.

Marehemu Seneta E. Kennedy wa Marekani aombolezwa na KM na UNHCR

Viongozi wa UM leo walitoa shukrani kadha na kumkumbuka kidhati seneta wa Marekani, Edward Kennedy ambaye alifariki Ijumanne usiku akiwa na umri wa miaka 77 baada ya kuugua saratani ya ubongo kwa muda mrefu.

Mabadiliko ya hali ya hewa yabatilisha historia kuwa ni kiashirio kwa wakulima, anasema Mkuu wa WMO

Michel Jarraud, Mkuu wa Shirika la UM juu ya Utabiri wa Hali ya Hewa Duniani (WMO) amenakiliwa akisema mabadiliko ya hali ya hewa yameifanya tarikh/historia kuwa ni chombo kisio sahihi tena katika kuongoza shughuli za wakulima, pamoja na wale wawekezaji wa kwenye nishati.

Mwanadamu anaweza kuambukiza mnyama A/H1N1, inasema WHO

Imetangazwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) ya kwamba kuna uwezekano kwa wanadamu, mara kwa mara, kuwaambukiza wanyama wa mifugo, kama nguruwe, kuku na mabata yale maradhi ya homa ya mafua ya aina ya A/H1N1.

Siku ya Kumbukumbu ya Kimataifa juu ya Taathira za Utumwa

Siku ya Kimataifa ya Kumbukumbu ya Ukomeshaji wa Biashara ya Utumwa huadhimishwa na UM kila mwaka mnamo tarehe 23 Agosti.