Americas

Wanariadha wa kimataifa kushiriki kwenye miradi ya kupiga vita njaa ulimwenguni

Jarno Trulli na Timo Glock, madereva wa mashindano ya mbio za gari, wenye kuwakilisha kampuni za Panasonic na Toyota, wanatazamiwa kuvalisha na kupamba gari zao na alama ya kitambulisho ya lile Shirika UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP), pale watakaposhiriki kwenye mashindano ya gari Uingereza mnamo Ijumapili ijayo.

WHO-UNICEF yasisitiza jitihadi kuu zahitajika kuhifadhi mahospitali na skuli penye maafa

Mashirika ya UM juu ya afya na maendeleo ya watoto, yaani mashirika ya WHO na UNICEF, yametoa mwito wa pamoja wenye kuzihimiza serikali za kimataifa, kuchukua hatua madhubuti, katika sehemu nne muhimu zinazohitajika kupunguza athari za maafa katika mahospitali na maskuli.

KM atoa mwito wa kuzikomesha chuki za kwenye uwanda wa intaneti

Ijumanne, kwa siku nzima mfululizo, Idara ya Habari ya UM kwa Umma (DPI) ilifanyisha warsha maalumu kuzingatia taratibu za kusitisha zile kurasa za mitandao ya kompyuta zenye kuchochea chuki.

Siku ya Dunia Kupiga Vita Kuenea kwa Jangwa

Tangu 1995 UM unaihishimu tarehe 17 Juni, kila mwaka, kuwa ni Siku ya Kupiga Vita Kuenea Kwa Jangwa. Ripoti za UM juu ya tatizo la kueneza majangwa, kutokana na matumizi badhirifu ya ardhi, inaashiria watu milioni 200 watalazimika kuhama makazi katika mwaka 2050 kutakakosababishwa na mabadiliko ya katika mazingira.

UNIDO na kampuni ya HP wafungua vituo vya mafunzo katika Afrika na Mashariki ya Kati

Shirika la UM juu ya Maendeleo ya Viwanda (UNIDO) ikishirikiana na kampuni ya teknolojiya ijulikanayo kama HP, yametangaza kufungua vituo 20 vya mafunzo katika Afrika na Mashariki ya Kati, vitavyotumiwa kuilimisha vijana wa umri wa baina ya miaka 16 mpaka 25, mafunzo yanayohusika na ujasiriamali na teknolojiya ya mawasiliano ya kisasa.

'Afya bora ndio msingi wa kufikia MDGs', asihi KM

Risala ya KM kufunga warsha maalumu kuhusu Afya ya Kimataifa kwenye mazingira ya mizozo, iliotolewa Ijumatano, ilisisitiza kwamba uwezo wa jumuiya ya kimataifa kuyafikilia, kwa wakati, yale Malengo ya Maendeleo ya Milenia, (MDGs) unafungamana kimsingi na matokeo mazuri kwenye zile juhudi za kuendeleza afya ya jamii.

'Watu milioni 42 waling'olewa makwao duniani 2008': UNHCR

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) leo imewasilisha ripoti ya mwaka ambapo imeeleza idadi ya watu waliolazimika kuyahama mastakimu, kwa sababu ya mateso, fujo na vurugu ulimwenguni, mnamo mwisho wa 2008, ilifikia wahamiaji milioni 42.

Nusu ya vifo vya barabarani huathiri wenda kwa miguu, wapanda baiskeli na wanaoendesha motosekli/pikipiki

Utafiti mpya uliofanywa na Shirika la Afya Duniani (WHO) umethibitisha ya kuwa nusu ya watu milioni 1.27 wanaokadiriwa kufariki kila mwaka kutokana na ajali za barabarani, ni watu wanaokwenda kwa miguu, na wale wanaopanda baiskeli na wanaoendesha motosekli/pikipiki.

Uongozi mpya unahitajika kukabiliana na mizozo ya ajira duniani. inasema ILO

Juan Somavia, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la UM juu ya Haki za Wafanyakazi (ILO) alipohutubia kikao cha ufunguzi wa Mkutano Mkuu juu ya Masuala ya Mizozo ya Ajira Duniani, uliofanyika Geneva, amependekeza kuwepo “uongozi mpya katika viwango vyote vya kiuchumi na kijamii" ili kusuluhisha vyema mizozo ya ajira kimataifa. Mkuu huyo wa ILO, alisema ulimwengu hauwezi tena kusubiri uchumi ukuwe, kwanza, kwa miaka kadha kabla ya kuamua kuzalisha ajira.

Mkuu wa WHO ahimiza haki kwenye sera za kimataifa

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Dktr Margaret Chan aliwaambia wajumbe wa kimataifa, waliohudhuria warsha maalumu uliofanyika Makao Makuu ya UM, kuwacha ile tabia ya “kuamini, bila kuelewa, madai yanayojigamba ustawi wa uchumi na natija zake kimataifa ndio mambo yatakayofanikiwa kumaliza na kuponya matatizo yote ya maisha duniani.”