Mapato ya fedha yasihatarishe maisha ya abiria na wafanyakazi wa ndege za kiraia- Mtaalamu
Mtaalamu maalum wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Agnès Callamard amesema kanuni za ulinzi wa ndege za kiraia zinazoruka kwenye maeneo ya mizozo ya kijeshi zisiwe na utata wowote na ziwe wazi ili kulinda maisha ya abira na wafanyakazi wa ndege hizo.