Aghanistan

UNAMA/Jawad Jalali (file)

Mashambulizi Afghanistan hayatokatisha tamaa wapiga kura

Umoja wa Mataifa umesema mashambulizi dhidi ya maeneo yanayohusika na masuala ya uchaguzi nchini Afghanistan yanachukiza.

Tamko hilo linafuatia mfululizo wa maeneo hayo ikiwemo vituo vya kusajili wapiga kura wakati huu ambapo uchaguzi unatarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu.

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa UN nchini humo Tadamicho Yamamoto amesema tangu kuanza kwa uandikishaji wapiga kura tarehe 14 mwezi huu raia 271 wameuawa katika matukio 23.

Sauti
1'53"