Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Afya ya uzazi

Mtoa huduma azungumza kuhusu afya ya uzazi na wanaume na wanawake. (Picha ya maktaba)
Diana Nambatya/Photoshare

Mradi wa uzazi wa mpango wa UNFPA kisiwani Unguja umeboresha hata mapenzi kati yetu-Othman Vuai

Na sasa tuelekee Kwarara Unguja, Zanzibar nchini Tanzania ambako shirika la idadi ya watu duniani, UNFPA limefadhili mradi wa ushirikishaji wa wanaume katika elimu ya afya ya Uzazi.

Afisa Mawasiliano mkuu wa UNFPA Tanzania, Warren Bright katika kukagua miradi hiyo kuangazia miaka 25 ya mafanikio ya mkutano wa kimataifa kuhusu idadi ya watu na maendeleo, ICPD uliofanyika Cairo, Misri mwaka 1994, amezungumza na Mwalimu Othman Maulid Vuai na mkewe Nargis Nassor ambao ni wanufaika wa mradi huo.

 

 

Sauti
2'9"
UN News/Grece Kaneiya

Jamii na serikali wanaitikia wito wa huduma za uzazi wa mpango

Vikao vya ngazi ya juu vya Umoja wa Mataifa vikiendelea kwenye makao makuu ya Umoja huo jijini New York, Marekani, mashirika ya kiraia nayo yanashiriki katika vikao vya kando kuelezea kile ambacho yanafanya mashinani kuchagiza malengo ya maendeleo endelevu, SDGs huko mashinani. Miongoni mwa mashirika  hayo ni lile la Restless Development nchini Tanzania ambalo kupitia mradi wa Tutimize ahadi linasaka takwimu kuangazia ni jinsi gani serikali inatekeleza ahadi za usawa wa kijinsia na mkakati wa uzazi wa mpango wa mwaka 2020.

Sauti
4'11"
Mama na mwana katika kituo cha kitaifa cha afya kwa ajili ya mama na mtoto, Ulaanbaatar, Mongolia.(Septemba 4, 2015)
UNICEF/Jan Zammit

Wanawake na watoto wanaishi zaidi leo hii kuliko awali – WHO/UNICEF

Wanawake zaidi na watoto wao kwa sasa wanaishi zaidi ya hapo awali kulingana na makadirio mapya ya watoto wanaokufa wakati wa kuzaliwa au kina mama wanaofariki dunia wakati wa kujifungua . Makadirio hayo yametolewa leo na mashirika ya Umoja wa Mataifa likiwemo la  kuhudumia Watoto duniani UNICEF na Shirika la Afya Duniani WHO.

Sauti
4'44"

24 Julai 2019

Katika Jarida la Habari hii leo arnold Kayanda anakuletea 

-Mikoko yaleta nuru kwa wakazi wa Pwani ya kenya licha ya kuhifadhi mazingira kwa kupunguza hewa ukaa yawaletea kipato wananchi kwa mujibu wa UN Environment

-Vijana nchini Tanzania wakumbatia mabadiliko ya kuachana na matumizi ya mifuko ya plastiki na kujipatia kipato kwa kutengeneza mifuko mbadala ya karatasi

-Elimu katika shule 25 nchini Kenya yapigwa jeki na mradi wa UNICEF wa  vitabu mtandaoni na matumizi ya Ipad

Sauti
13'35"