Afrika ya Kati

Zuia ndoa za utotoni kuokoa maisha ya wasichana :UNICEF

Unaelewa nini unaposikia kutoka kwenye vyombo vya habari au sehemu mbali mbali watu wakisema ndoa za utotoni?, tuungane na Flora Nducha anayetuambia maana yake, hali ilivyo ulimwenguni na nini kifanyike kuzitokomeza.

Uwasiishaji wa silaha ni ishara mzuri kuelekea amani eneo la PK5, Bangui

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kuweka amani na utulivu nchini Jamhuri ya Afrika ya kati

Sauti -
2'5"

Nuru ya amani yaanza kuonekana katika eneo la PK 5, MINUSCA yashuhudia 

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kuweka amani na utulivu nchini Jamhuri ya Afrika ya kati MINUSCA, umewapongeza waliokuwa wanachama wa makundi ya wapiganaji katika eneo la PK 5 waliokuwa wanajiita makundi ya kujilinda baada ya kukabidhi silaha zao mbele ya Waziri wa nchi hiyo anayesimamia upokonyaji silaha kutoka kwa raia, ujumuishaji na urejeshaji katika jamii wa watu waliokuwa wapiganaji ikiwa ni sehemu za Umoja wa Mataifa kuhamasisha usitishaji mapigano duniani kote.

Ukatili umesababisha zaidi ya watoto milioni 1.9 kusitisha masomo magharibi na Afrika ya Kati-UNICEF

Zaidi ya watoto milioni 1.9 wamelazimika kukatisha masomo yao magharibi na Afrika ya kati kwa sababu ya ongezeko la mashambulizi na vitisho vya kikatili dhidi ya elimu katika ukanda huo, imesema ripoti ya Shrikia la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF leo Ijumaa.

Tungearifiwa tungeshiriki mkutano leo kuhusu Afrika ya Kati:DRC

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, imesema imeamua kutoshiriki mkutano maalumu wa ngazi ya juu wa mawaziri ulioandaliwa kandoni mwa mjadala wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu masuala yanayolighubika eneo la Afrika ya Kati ikiwemo DRC.