Afrika Kusini

Vijana mkidhamiria mnaweza kukabiliana na chochote:Amina J. Mohammed

Vijana barani Afrika wameaswa kudhamiria kukabiliana na changamoto zinazowakabili na pia kuikabili duniani , kwani penye nia pana njia. Wito huo umetolewa leo na naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina J. Mohammed katika mkutano wa maendeleo ya vijana barani Afrika unaofanyika mjini Johannesburg nchini Afrika Kusini.

Uwekezaji ugenini wapungua, nchi zinazoendelea hazikuathirika- UNCTAD

Uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni, FDI, ambao hutajwa kama kichocheo kikubwa cha ukuaji wa uchumi duniani, umeporomoka kwa zaidi ya asilimia 40 katika nusu ya kwanza yam waka huu wa 2018.

Vijana wa sasa si wa kusubiri kufunguliwa milango- Rais Ramaphosa

Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini amehutubia mjadala mkuu wa Baraza la Kuu la Umoja wa Mataifa ikiwa ni mara ya kwanza tangu achaguliwe kushika wadhifa huo akisema kuwa vijana wa sasa si wale wa kusubiri kufunguliwa milango.

Dunia ijifunze kusamehe kama alivyofanya Mandela- Balozi Mero

Leo katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani, nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa wanapitisha azimio la kumuenzi aliyekuwa Rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini, Hayati Nelson Mandela.

Afrika Kusini na mwelekeo sahihi kupambana na Ukimwi


Ushahidi zaidi kutoka Cameroon, , Côte d’Ivoire, na Afrika Kusini umezidi kudhihirisha mwelekeo sahihi wa dunia katika kukabiliana na Ukimwi ifikapo mwaka 2020.

Ujerumani, Indonesia, Afrika Kusini, miongoni mwa wajumbe wapya baraza la Usalama

Baraza kuu la Umoja wa Mataifa leo Ijumaa limewachagua wajumbe watano wapya wa baraza la usalama wasio wa kudumu.

Winnie Mandela-shujaa aliyebeba mkuki kutetea wanyonge

Winnie Nomzamo  Madikizela Mandela! aliaga dunia mwezi huu wa Aprili! Daima atakumbukwa kwa harakati zake za ukombozi wa taifa la Afrika Kusini dhidi ya  ukatili wa ubaguzi wa rangi ulioshamiri nchini humo karne ya 20. Ma Winnie kama alivyojulikana zaidi licha ya taswira yake kukumbwa na misukosuko wakati wa uhai wake, kifo chake kiligeuka fursa kwa watu wengi kuweza kumfahamu zaidi na kujifunza tofauti na mengi maovu yaliyosemwa wakati wa uhai wake.

Sauti -
3'58"

Kwaheri Winnie Mandela umeacha pengo lisilozibika katika haki: Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema taarifa za msiba wa mwanaharakati wa kupigania haki za binadamu na kupinga ubaguzi wa rangi Winnie Madikizela Mandela uliotokea mapema leo umemshitua na kumgusa sana.

Sauti -
1'30"

Kwaheri Winnie Mandela umeacha pengo lisilozibika katika haki:Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema taarifa za msiba wa mwanaharakati wa kupigania haki za binadamu na kupinga ubaguzi wa rangi Winnie Madikizela Mandela uliotokea mapema leo umemshitua na kumgusa sana.

Kinachosikitisha zaidi ubaguzi wa rangi na chuki vinaendelea:Guterres

Mifumo yote ya ubaguzi wa rangi, chuki dhidi ya wageni na kutovumiliana ni lazima iendelee kupingwa vikali kote duniani. Wito huo umetolewa jumanne na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, katika mjadala maalumu ya maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kutokomeza ubaguzi wa rangi uliofanyika kwenye baraza kuu la umoja wa Mataifa  mjini New York Marekani.

Sauti -
2'12"