Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

2017

UN News/Maoqi Li

Hatujawasahau wana CAR- Mueller

Naibu Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu, OCHA, Ursulla Mueller, anaendelea na ziara yake ya siku nne nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR.

Katika siku yake ya pili ya ziara hiyo hii leo amekuwa na mazungumzo na viongozi wa mashirika ya misaada ya kibinadamu ikiwemo lile la madaktari wasio na mipaka, MSF kwenye mji mkuu, Bangui.

Bi. Mueller amepongeza uwepo thabiti wa MSF nchini humo akitaja miradi 12 ambayo shirika hilo inatekeleza katika majimbo 10 ya CAR.

Sauti
1'20"
UN News/Patrick Newman

Nachukizwa sana na wanaoona wenye shida ni ombaomba- Brenda

Kwa siku nne kuanzia tarehe 8 Februari 2018 vijana kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa walikutana jijini New York, Marekani kwa ajili ya mjadala wa mustakhbali wa dunia. Mjadala huo wa vijana umefanyika kwa kuzingatia mfumo wa Umoja wa Mataifa, ikiwa ni mojawapo ya njia ya kuwandaa vijana kubeba jukumu la kusongesha maendeleo kwenye nchi zao na dunia kwa ujumla. Miongoni mwao ni Brenda Kimwatan, mwanafunzi kutoka Kenya ambaye anasoma Chuo Kikuu cha Cape Town nchini Afrika Kusini.

Sauti
4'10"

Idadi ya watalii duniani ilipanda 2017 na huenda ikaongezeka zaidi :UNWTO

Idadi ya watalii wa kimataifa, wanaowasili katika nchi nyingine, na watu wanaoingia nchi moja kwa siku kwa njia  halali iliongezeka mwaka wa 2017 kwa kiwango cha asili mia 7 na na hivyo  kufikia watalii Zaidi ya millioni elfu moja na mia tatu.

Hii ni kwa mujibu wa vigezo vipya vya shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii duniani UNWTO. Shirika hilo linabashiri kuwa ongezeko hilo litazidi kuvuma mwaka 2018 kwa kiwango cha asili mia  kati ya nne na tano.