Jumuiya ya kimataifa yahimizwa kuisaidia Ukraine wakati huu msimu wa baridi kali ukianza
Mcheza filamu maarufu duniani Nikolaj Coaster-Waldau anayefahamika zaidi kwa kuigiza katika filamu ya Game of Thrones ambaye pia ni Balozi Mwema wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo Duniani UNDP ametembelea nchini Ukraine kujionea hali ilivyo wakati huu ambao mapigano baina ya Urusi na Ukraine yakiendelea.
Muigizaji huyo Nikolaj Coster- Waldau ametembekea katika mji wa Kyivv nchini Ukraine ambao umeathiriwa vibaya ya makombora ya jeshi la Urusi ambayo mbali na kuharibu makazi ya watu, pia yameharibu miundombinu ya umma.
Ziara hii ya takriban wiki moja inakuja kipindi hiki ambacho wananchi wa Ukraine wanashuhudia mwaka wao wa Tano wa msimu wa baridi katikati ya mapigano. Waldau anasema
"Kyivv ni mji mkubwa na wenye baridi kali na unakuhitaji kupata joto, kupata joto ni moja ya hitaji la msingi la kibinadamu na utu wa mwanadamu na maisha."
Alitembelea na kujionea maisha ya wananchi ambao wengi wanakabiliwa na hali tete ya uhakika wa nishati itakayoweza kuwapa joto katikati ya baridi kali.
Baada ya kuzungumza na wananchi, Nikolaj Coster-Waldau akatoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kusaidia kuhakikisha nishati ya umeme na miundombinu ya kupeleka joto inapatikana katika msimu huu wa baridi kali
"Natumaini tutaweza kutoa msaada wa kimataifa wakutosha kuwezesha UNDP kwenda kuwasaidia kuleta mabadiliko na kuboresha usambazaji wa umeme katika gridi kuu kwakuwa hilo ndio hitaji kwani kwa sasa mfumo unahali tete."
Muigiza filamu huyu pia alitembelea katika mitambo ya kusambaza joto ambapo mwaka jana UNDP ilifanikiwa kuboresha na kurejesha mitambo yakusambaza joto ambapo watu zaidi ya milioni 6.6 walinufaika, hata hivyo shirika hilo linahitaji msaada zaidi.
Oleksii Nazarenko ni msimamizi kiongozi wa timu ya kufanya marekebisho ya dharura wa UNDP mjini Kyivv.
"Vituo vyetu vya nishati na miundombinu ya kusambaza joto vipo katika hatari kubwa, unajua, ni vigumu kuwa tumejiandaa kikamilifu, au kuwa tumejilinda kwa asilimia 100 dhidi ya mashambulizi."
Jumuiya za kimataifa zinaombwa kuisaidia Ukraine katika msimu huu wa baridi kali.