Kauli ya Guterres kuhusu tukio la FlyDubai
Kauli ya Guterres kuhusu tukio la FlyDubai
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameelezea wasiwasi wake mkubwa kuhusiana na tukio katika ndege ya shirika la ndege la FlyDubai iliyokuwa inasafiri kuelekea Tel Aviv nchini Israeli ikitokea Falme za Kiarabu.
Tukio hilo, kwa mujibu wa vyombo vya habari, linadaiwa kuhusisha marubani wawili waliokuwa wanaendesha ndege hiyo, ambapo mmoja wao yadaiwa alikuwa anajaribu kumchoma rubani mwenzake kisu, hali iliyosababisha msukosuko hadi wafanyakazi wengine wa ndege na abira kuingilia kati.
Kupitia taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani Jumatano usiku, Katibu Mkuu ameshukuru kwamba janga ambalo lingaliweze kutokea, liliepukika.Ndege hiyo iliweza baadaye kutua mji wa Tabuk nchini Saudi Arabia.
“Nalaani vikali kitendo chochote kinachoweka hatarini maisha raia na usalama wa anga,” amesema Katibu Mkuu.
Halikadhalika ametoa shukrani zake kwa mamlaka husika kwa kuhakikisha usalama wa raia wote na kwa uchunguzi uliofanyika huku akisema kwamba, “tutaendelea kufuatilia yale yote yanayohusiana na tukio hilo.”