Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zambia: Kamishna wa Haki za Binamu wa Umoja wa Mataifa aguswa na ukamatwaji wa wapinzani

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari huko Geneva.
UN Photo/Loey Felipe Volker Türk Kamishina Mkuuwa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa (Maktaba)

Zambia: Kamishna wa Haki za Binamu wa Umoja wa Mataifa aguswa na ukamatwaji wa wapinzani

Haki za binadamu

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Türk, amesema ana wasiwasi kuhusu taarifa za kukamatwa na kuzuiliwa kwa wanachama wa vyama vya upinzani nchini Zambia kabla na baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika Agosti 13 katika ncho hiyo ya barani Afrika.

Katika taarifa iliyotolewa leo na ofisi yake mjini Geneva, Uswisi, Türk ametoa wito kwa mamlaka za Zambia kuhakikisha kuwa ukamataji wote na hatua za kisheria zinazofuata zinaendana kikamilifu na viwango vya kimataifa vya haki za binadamu pamoja na sheria za Zambia.
 
“Nina wasiwasi kuhusu taarifa za kukamatwa na kuzuiliwa kwa wanachama wa upinzani nchini Zambia kabla na baada ya uchaguzi mkuu wa Agosti 13,” imemnukuu taarifa iliyotolewa na ofisi yake leo Agosti 19.
 

Acheni ukamataji holela

 
Amesisitiza kuwa mamlaka zinapaswa “kuacha kuwakamata watu kiholela na kuheshimu kikamilifu haki za kisheria za wote wanaozuiliwa.”
 
Türk pia ametoa wito kwa mamlaka kuhakikisha kuwa kila anayekamatwa anafahamishwa mara moja sababu za kukamatwa kwake na mashtaka yanayomkabili, anapewa fursa ya kupata uwakilishi wa kisheria na kuwasiliana na familia yake, na anatendewa kwa utu akiwa kizuizini.
 
Amesema pia ni muhimu kuhakikisha kuwa waliokamatwa wanafikishwa mbele ya hakimu bila kuchelewa na wanapata njia madhubuti za kudai haki iwapo haki zao zimekiukwa.
 
“Katika kipindi hiki muhimu baada ya uchaguzi, ni muhimu kuheshimu haki za binadamu na kuhakikisha kuwa malalamiko yoyote yanayotokana na uchaguzi yanaelezwa na kushughulikiwa kwa amani, na kwa kuzingatia sheria za kimataifa za haki za binadamu,” amesema Türk.