Tunawapatia huduma na twatumai wote watapona- Daktari wa Ebola DRC
Kulingana na ripoti mpya kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa, mlipuko wa sasa wa Ebola ya Bundibugyo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, (DRC) umekuwa mmoja wa milipuko mibaya zaidi kuwahi kutokea nchini humo. Huko Bunia, jimboni Ituri ambako ni kitovu cha mlipuko wa sasa wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu wakiwemo madaktari wanaongeza juhudi zao za kuwahudumia wagonjwa wakati huu ambapo ripoti zinasema watu zaidi ya 500 wamepona Ebola ya sasa.
Priscilla Lecomte aliyeko kwenye timu ya Mratibu Mkuu wa Ebola wa Umoja wa Mataifa, Julien Harneis, amezungumza na mmoja wa madaktari.
Asemavyo Dkt. Martin
- Yeye ni mwenyeji wa Bunia
- Ni mara ya kwanza kutibu wagonjwa wa Ebola
- Kutokana na joto wanatakiwa kuhudumia kwa nusu saa
- Baada ya nusu saa wanapumzika
- Na kisha wanarejea tena kwenye chumba cha matibabu
- Wanatakiwa kuhudumia kwa muda wa jumla ya saa moja au moja na nusu
- Hana hofu yoyote na wala hana changamoto yoyote kwani mipango imewekwa sawa
- Matumaini yake ni kwamba wagonjwa watapona
Takwimu za Umoja wa Mataifa zinaonesha kuwa wagonjwa zaidi ya 500 walioambukizwa Ebola wakati wa mlipuko wa sasa wa Ebola, DRC wamepona.
Harakati za kuelimisha umma zinaendelea kwenye majimbo matatu yenye mlipuko wa sasa ambayo ni Kivu Kaskazini, Kivu Kusini na Ituri.
Bunia, mji mkuu wa Ituri ndio kitovu cha mlipuko wa sasa uliotangazwa rasmi mwezi Mei mwaka huu wa 2026