Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sura ya 6 ya Katiba ya Umoja wa Mataifa yamulikwa Barazani ili kuimarisha upatanishi

Mwanamume aliyevaa shati la WFP anapatanisha mgogoro wa kinyumbani ofisini huku wanajamii wengine wakifuatilia.
UN News Kikao cha upatanishi wa mzozo wa nyumbani kwenye ofisi yakongozi wa wakimbizi kyangwali nchini Uganda.

Sura ya 6 ya Katiba ya Umoja wa Mataifa yamulikwa Barazani ili kuimarisha upatanishi

Amani na Usalama
  • Inahusu nini?
  • Ni kwa vipi inaweza kuimarisha upatanishi?
  • Katibu Mkuu ametoa mapendekezo yapi?

MAPENDEKEZO YA KATIBU MKUU

  • Kuimarisha upatanishi wa Umoja wa Mataifa.

Kwa kupanua diplomasia ya kuzuia migogoro.

  • Kuimarisha diplomasia ya kikanda.

kwa kutumia kikamilifu ofisi za kikanda za Umoja wa Mataifa.

  • Baraza la Usalama lichukue hatua mapema.

kwa kutumia hatua za kuzuia migogoro.

  • Kuongeza juhudi za kubaini ukweli.

Kwa kuimarisha uchunguzi.

  • Kukuza mchakato shirikishi wa amani.

Kwa kujumuisha wanawake, vijana na asasi za kiraia.

  • Kuhamasisha ushiriki mkubwa wa nchi wanachama.

Kwa kuzitaka zote ziunge mkono upatanishi.

Sura ya 6 ya Katiba ya Umoja wa Mataifa inahusu utatuzi wa migogoro kwa njia za amani, na inaipa Baraza la Usalama mamlaka ya kuzitaka pande zinazohusika katika mgogoro kuutatua kwa amani kabla haujahatarisha amani na usalama wa kimataifa.

Hivyo mjadala unalenga:

  • Kubaini mbinu bora na upungufu uliopo kwenye mifumo ya utatuzi wa migogoro inayotokana na Katiba hiyo.
  • Kuchunguza jinsi diplomasia na upatanishi vinavyoweza kujenga kuaminiana na kuzuia migogoro.
  • Kutathmini utekelezaji wa Azimio 2788  la mwaka 2025, ambalo lilimtaka  Katibu Mkuu kutoa mapendekezo ya kuimarisha zaidi mifumo ya utatuzi wa migogoro kwa njia za amani mwaka mmoja baada ya kupitishwa kwake.

Katiba ya UN ni tumaini la binadamu- Guterres

Mkutano wa leo ulioitishwa na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC pamoja na Pakistani, uliongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa DRC Thérèse Kayikwamba Wagner.

Katika hotuba yake kama ambavyo azimio namba 2788 linasema, Katibu Mkuu Antonio Guterres alitoa tathmini ya hali ya amani duniani na madhara yake kwa wakazi wa dunia.

“Migogoro ya Mashariki ya Kati, Gaza, Ukraine, Sudan na Sahel inaonesha kuwa nguvu za kijeshi hazileti suluhisho la kudumu, huku raia wakiendelea kuathirika zaidi. Diplomasia ndiyo njia pekee ya kufikia amani ya kudumu,” amesema Guterres.

Ameliomba Baraza la Usalama kuongeza juhudi za kutatua migogoro kwa njia ya amani, akionya kuwa dunia inakabiliwa na ongezeko la vita, ukiukwaji wa sheria za kimataifa na kupungua kwa imani katika diplomasia.

Bofya video kutazama hotuba ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa