Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mjadala wa wazi wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu usimamizi wa rasilimali asili

Wachimbaji madini wa kienyeji hubeba magunia makubwa ya madini kwenye kilima chenye miamba katika mgodi wa Mudere katika eneo la Kivu Kaskazini mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
© Adobe Stock/Erberto Zani Kobalti inachimbwa huko Rubaya, mashariki mwa Congo, eneo linalodhibitiwa na wanamgambo.

Mjadala wa wazi wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu usimamizi wa rasilimali asili

Amani na Usalama

Swali kuu lilikuwa katika kikao hicho cha Baraza la Usalama lilikuwa: Je, utajiri huu wa madini utachangia kujenga amani na ustawi, au utafadhili migogoro na rushwa?

Mambo muhimu yaliyojitokeza kwenye Mjadala huu wa Wazi wa Ngazi ya Juu ulioitishwa na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, (DRC) kuangalia maliasili au rasilimali asili na mchango wake katika kuendeleza amani ni kama ifuatavyo.

  • Madini ya kimkakati, madini adimu na maliasili kama misitu ni muhimu katika kuendeleza maendeleo ya kijamii
  • Usimamizi na utawala bora ni muhimu katika kuhakikisha rasilimali hizo asilia zinanufaisha kila mwananchi
  • Maliasili hizo ziongezewe thamani kwenye nchi husika badala ya kusafirishwa ghafi kwenda nchi za nje.
  • Kuelekea mpito wa nishati safi, bila usimamizi sahihi wa rasilimali hizo nchi maskini zitajikuta masikini wa nishati licha ya kuwa na utajiri mkubwa wa maliasili hizo.

🔴BOFYA PICHA KUTAZAMA KILICHOENDELEA