Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mchango wa Chuo Kikuu cha Mount Kenya katika kutekeleza UN SDG 9

Mwanamume aliyevaa suti amesimama mbele ya bango la Jukwaa la Kisiasa la Ngazi ya Juu kuhusu Maendeleo Endelevu katika Chuo Kikuu cha Mt. Kenya.
UN News/Anold Kayanda Profesa Peter Wanderi Mwangi ambaye amewakiwakilisha Chuo Kikuu cha Mount Kenya cha nchini Kenya chenye matawi mbalimbali katika Afrika Mashariki katika mkutano wa United Nations Academic Impact (UNAI), Mpango unaosisitiza nafasi muhimu ya taasisi za elimu ya juu katika kuhimiza maendeleo endelevu na kuunga mkono utekelezaji wake.

Mchango wa Chuo Kikuu cha Mount Kenya katika kutekeleza UN SDG 9

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Umoja wa Mataifa ili kuyafikia Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) kama ilivyopangwa yawe yamefanikiwa kufikia mwaka 2030, waliona ni muhimu pia kuhusisha taasisi za kitaaluma duniani ndipo wakaja na kile kwa lugha ya Kiingereza walikiita ‘United Nations Academic Impact (UNAI)’, mpango unaosisitiza nafasi muhimu ya taasisi za elimu ya juu katika kuhimiza maendeleo endelevu na kuunga mkono utekelezaji wake.

Baadaye vilianzishwa vituo vya mpango huo ambavyo kila kimoja kilipewa lengo la kusongesha. Vyuo Vikuu hivyo vilivyoko katika mpango huu vimefanya Kongamano la Kimataifa kuhusu Elimu ya Juu na kimojawapo ni Chuo Kikuu cha Mount Kenya cha nchini Kenya chenye matawi mbalimbali katika Afrika Mashariki. Chuo Hiki kilichukua jukumu la kutekeleza lengo namba 9 linalolenga kuendeleza viwanda, ubunifu na miundombinu.

Mjadala wa jopo katika Makao Makuu UN jijini New York, huku ujumbe wa Kenya ukizungumza na hadhira.
UN News/Anold Kayanda Kongamano la United Nations Academic Impact (UNAI), Mpango unaosisitiza nafasi muhimu ya taasisi za elimu ya juu katika kuhimiza maendeleo endelevu na kuunga mkono utekelezaji wake, lililofanyika kandoni mwa mkutano wa HLPF katika Makao Makuu UN jijini New York.

Profesa Peter Wanderi Mwangi ni mmoja wa washiriki wa mkutano huo amewakiwakilisha chuo hicho katika mkutano huo  uliofanyika kandoni mwa Jukwaa la Kisiasa la Ngazi ya Juu kuhusu Maendeleo Endelevu (HLPF) linalohitimishwa kesho hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York Marekani. Profesa Wanderi anaeleza wanavyochangia kusongesha SDGs.

Audio file