Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lakutana tena kujadili vikwazo vya Marekani dhidi ya Cuba

Matokeo ya upigaji kura yanaonyeshwa kwenye skrini kubwa katika Baraza Kuu UN wakati wa kupiga kura kuhusu marufuku ya Marekani dhidi ya Cuba.
Picha ya UN/Manuel Elías Baraza Kuu la UN lapiga kura kuhusu umuhimu wa kukomesha vikwazo vya kiuchumi, kibiashara na kifedha vilivyowekwa na Marekani dhidi ya Cuba.

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lakutana tena kujadili vikwazo vya Marekani dhidi ya Cuba

Ukuaji wa Kiuchumi

Asubuhi hii ya Julai 7 kwa saa za New York Marekani, kwa mara ya 34 tangu mwaka 1992, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limekaa ili kujadili umuhimu wa kumaliza vikwazo vya kiuchumi na kibiashara vilivyowekwa na Marekani dhidi ya Cuba tangu mwaka 1960.

Katika barua ya mwaliko ambayo Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Annalena Baerbock amewapelekea wajumbe wa Baraza anasema, “ninayo heshima kukujulisha kwamba nimepokea barua kutoka kwa Mhe. Bwana Ernesto Soberón Guzmán, Mwakilishi wa Kudumu wa Cuba katika Umoja wa Mataifa, akiomba kuitishwa kwa kikao cha Baraza Kuu ili kujadili ajenda namba 38 yenye kichwa: “Umuhimu wa kukomeshwa kwa vikwazo vya kiuchumi, kibiashara na kifedha vilivyowekwa na Marekani dhidi ya Cuba.”

Mwanaume anavuka barabara katika mtaa wa Old Havana, jijini Havana, mji mkuu wa Cuba.
© Unsplash/Carlos Torres Mwanaume anavuka barabara katika mtaa wa Old Havana, jijini Havana, mji mkuu wa Cuba.

Kikao cha namna hii mara ya mwisho kilifanyika tarehe 28 na 29 mwezi Oktoba mwaka jana 2025.

Unaweza kufuatiliaa mjadala huo kwa kubofya hapa.