Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanachama watano wapya wasio wa kudumu wa Baraza la Usalama wachaguliwa

Mkutano mkuu wa Baraza Kuu UN kwa ajili ya uchaguzi wa wanachama wasio wa kudumu wa Baraza la Usalama, huku wajumbe wakiwa wameketi ukumbini na nembo UN ikionekana ukutani.
UN Photo/Manuel Elías Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipochagua wajumbe watano wapya wasio wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mwaka 2025. Wajumbe hao wanamaliza mihula yao miwili mwaka huu na wanachaguliwa wengine.

Wanachama watano wapya wasio wa kudumu wa Baraza la Usalama wachaguliwa

Masuala ya UM

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limechagua wanachama watano wapya wasio wa kudumu wa Baraza la Usalama kwa muhula wa 2027–2028 katika uchaguzi utakaofanyika asubuhi hii ya Jumatano ya Juni 3,2026.

Nchi zilizochaguliwa ni Austria, Ureno, Zimbabwe, Trinidad na Tobago ingawa upigaji kura unaendelea kwa kiti kimoja kilichobaki cha Mataifa ya Asia-Pasifiki
 
Ujumbe wa Zimbabwe unasherehekea kuchaguliwa kama mwanachama asiye wa kudumu wa Baraza la Usalama.
Picha ya UN/Eskinder Debebe Ujumbe wa Zimbabwe unasherehekea kuchaguliwa kama mwanachama isiye wa kudumu wa Baraza la Usalama kwa muhula wa miaka miwili kuanzia Januari 2027.

Taarifa za hivi punde

 
Hatimaye baada ya mizunguko mitatu ya marudio ya kura, Kyrgyzstan imeshinda kwa kupata kura 142 didi ya 49 za Ufilipino kwa hiyo Kyrgyzstan imejiunga na Austria, Ureno, Zimbabwe, Trinidad na Tobago kuwa wajumbe watano wa wasio wa kudumu wa Baraza la Usalama kwa kipindi cha miaka miwili ijayo.
 

Idadi ya kura

Austria imepata kura 141 na Ureno imepata kura 144, hivyo nchi hizo mbili zikapata viti vya Kundi la Ulaya Magharibi na Nyinginezo (WEOG). Ujerumani haikuchaguliwa kwani imeambuliwa kura 104.

Wajumbe kutoka Trinidad na Tobago washerehekea ushindi katika mkutano wa Baraza la Usalama UMOJA WA MATAIFA , wakishikana mikono katika chumba cha bunge.
Picha ya UN/Eskinder Debebe Ujumbe wa Trinidad na Tobago unasherehekea kuchaguliwa kama mjumbe isiye wa kudumu wa Baraza la Usalama kwa muhula wa miaka miwili kuanzia Januari 2027.

Katika makundi ya Afrika na Amerika ya Kusini pamoja na Karibe, Trinidad na Tobago imepata kura 181, na Zimbabwe kura 182, hivyo zikashinda viti vyao.

Ili kuchaguliwa, mgombea anahitaji kupata theluthi mbili ya wanachama waliopo na wanaopiga kura, ambayo katika hali hii ni kura 127. Sasa kwa kuwa kiti cha Asia-Pasifiki Kyrgyzstan imepata kura 105 na Ufilipino ikapata kura 85 kwa msingi huo hakuna kati yao aliyefikia kizingiti hicho, hivyo duru zaidi za upigaji kura zinahitajika.

 
Nchi hizi zilizochaguliwa zitahudumu kwa kipindi cha miaka miwili kuanzia tarehe 1 Januari 2027 hadi 31 Desemba 2028, na zimechukua nafasi za Somalia, Pakistan, Panama, Denmark na Ugiriki, ambazo mihula yao itaisha mwishoni mwa mwaka huu 2026.
Nchi zilizochaguliwa ni
 

Makundi ya Kikanda

 
Jumla ya nchi saba zilikuwa zimewania nafasi tano katika makundi mbalimbali ya kikanda. Austria, Ujerumani na Ureno zinashindania nafasi mbili zilizotengwa kwa Kundi la Mataifa ya Ulaya Magharibi na Nchi Nyingine (WEOG), huku Kyrgyzstan na Ufilipino zikishindania nafasi moja iliyotengwa kwa Kundi la Asia na Pasifiki.
 
Wajumbe kutoka Zimbabwe washerehekea kuchaguliwa kwao kama mwanachama asiye wa kudumu wa Baraza la Usalama UN .
Picha ya UN/Eskinder Debebe Ujumbe wa Zimbabwe unasherehekea kuchaguliwa kama mwanachama isiye wa kudumu wa Baraza la Usalama kwa muhula wa miaka miwili kuanzia Januari 2027.
Katika makundi ya Afrika na Amerika ya Kusini pamoja na Karibe, Zimbabwe na Trinidad na Tobago zimegombea bila wapinzani. Hali hiyo ilifanya mijadala na ushindani mkubwa kuelekezwa katika makundi ya Ulaya Magharibi na Asia-Pasifiki, ambako nchi kadhaa ziliwania nafasi chache zilizopo.
 

Mara ya kwanza

 
Uchaguzi huu una umuhimu wa kipekee kwa Kyrgyzstan, ambayo haijawahi kuwa mwanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Ikiwa itachaguliwa, itakuwa mara ya kwanza kwa taifa hilo la Asia ya Kati kuhudumu katika chombo hicho chenye jukumu la msingi la kudumisha amani na usalama wa kimataifa. Ufilipino nayo inalenga kurejea katika Baraza hilo baada ya kuhudumu katika vipindi vya awali.
 
Baraza la Usalama lina jumla ya wanachama 15, wakiwemo wanachama watano wa kudumu na wanachama 10 wasio wa kudumu wanaochaguliwa na Baraza Kuu kwa mihula ya miaka miwili inayopishana. Uchaguzi hufanyika kila mwaka ili kujaza nafasi za wanachama watano wanaomaliza muda wao wa kuhudumu, hatua inayolenga kuhakikisha uwakilishi wa kikanda na mwendelezo wa kazi za Baraza katika kudumisha amani na usalama duniani.
 
Ujumbe wa Kyrgyzstan unasherehekea kuchaguliwa kama mjumbe asiye wa kudumu wa Baraza la Usalama katika UMOJA WA MATAIFA huko New York.
Picha ya UN/Eskinder Debebe Ujumbe wa Kyrgyzstan unasherehekea kuchaguliwa kama mjumbe isiye wa kudumu wa Baraza la Usalama kwa muhula wa miaka miwili kuanzia Januari 2027.

Hatimaye

 
Hatimaye baada ya mizunguko mitatu ya marudio ya kura, Kyrgyzstan imeshinda kwa kupata kura 142 didi ya 49 za Ufilipino kwa hiyo Kyrgyzstan imejiunga na Austria, Ureno, Zimbabwe, Trinidad na Tobago kuwa wajumbe watano wa wasio wa kudumu wa Baraza la Usalama kwa kipindi cha miaka miwili ijayo.