Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtu wa kwanza kutoka 'dunia ya kusini' kuongoza nafasi ya juu UNOCHA, Joyce Msuya astaafu

Joyce Msuya wa UNOCHA anakutana na mamlaka za mitaa huko Birao, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Oktoba 2025.
© UNOCHA/Virginie Bero Birao, Jamhuri ya Afrika ya Kati Oktoba 2025. ASG, Joyce Msuya (kushoto), wakati wa misheni yake katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, anakutana na serikali za mitaa.

Mtu wa kwanza kutoka 'dunia ya kusini' kuongoza nafasi ya juu UNOCHA, Joyce Msuya astaafu

Msaada wa Kibinadamu

Mwisho wa wiki hii, Mei 31, 2026, Joyce Msuya, raia wa Tanzania ambaye pia amewahi kuhudumu katika Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo, UNEP na pia Benki ya Dunia anahitimisha utumishi wake katika Umoja wa Mataifa akiwa Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya kibinadamu na pia Naibu wa Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Misaada ya Kibinadamu (OCHA).

Katika mazungumzo haya na Anold Kayanda wa Idhaa hii, Joyce Msuya anaanza kwa kuitafari miaka minne aliyohudumu katika nafasi hii.

Nikiangalia miaka minne iliyopita vitu vitatu vinakuja kwenye fikra zangu. Kwanza ni mhumi kukumbuka nilichukua hii kazi siku sita kabla ya vita vya Ukraine havijaanza. Na hiyo ilikuwa ni mwezi wa pili (Februari) mwaka 2022 na pili viya vya Gaza. Kuacha changamoto nyingine amvazp zilikuwepo kama za Sudan, DRC na vitu kama hivyo. Kwa hiyo kwanza ni kuona kazi ya Umoja wa Mataifa ambayo ni ngumu sana hasa ya OCHA kuangalia usalama wa binadamu. Na hapa mwishoni kuona hivi vita vya Iran. La pili ni heshima kwani mimi ni mtu wa kwanza kutoka ‘dunia ya kusini’ kushika nafasi hii katika OCHA.

Naibu Katibu Mkuu wa UNOCHA Joyce Msuya anasoma na watoto ndani ya hema katika Kambi ya Al Sumya ya Wadudu (IDP) huko Yemen.
© UNOCHA Mji wa Marib. Msaidizi wa Katibu Mkuu Msaidizi wa Masuala ya Kibinadamu, Joyce Msuya akiwa amekaa na Mwanafunzi wa Shule ya Al Naser ndani ya hema alipotembelea Kambi ya Al Sumya IDP iliyopo Marib nchini Yemen tarehe10-10-2022.
Umetembelea zaidi nchi 30 na tulikuwa tunaona ukizungumza na watu katika shida, ni simulizi gani unaikumbuka imebaki kwenye moyo wako?

Kwanza ni ukarimu wa watu ambao na binadamu ambao wameteseka sana. Naweza nikakupa hadithi moja nilikuwa ninatembelea kambi za wakimbizi Yemen.Kuna mama ambaye alikuwa na watoto wanne akanikaribisha kwake na nilikuwa sijui ni kitu gani cha kutegemea. Akaniambia maisha yake yote alikuwa na miaka kama thelatini na mbili hajawahi kuishi sehemu moja amekuwa anahama yeye na watoto wake, anajifungu akiwa njiani. Lakini kitu ambacho ninakumbuka kuhusu ukarimu wake alinikaribisha kwenye hema lake ambalo alikuwa amepewa na UNHCR, asubuhi hiyo alikuwa ameenda shambani kutafuta kitu kunikaribisha mimi nyumbani kwake. Kwa hiyo akanipa vinyanya vitatu nakumbuka vidogo tukakaa chini kwenye udongo lakini ule ukarimu kwamba pamoja na shida zote ametoka akaenda kutafuta nyanya kunikaribisha kwake...

Naibu Katibu Mkuu wa UNOCHA Joyce Msuya akifanya mahojiano ya kuondoka na mwanamke na mtoto wake huko Zémio, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Oktoba 2025.
Maxime Nama Zémio, Jamhuri ya Afrika ya Kati Oktoba 2025. ASG, Joyce Msuya, wakati wa misheni yake katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, katika tarafa ya Zémio, Kusini mwa Mashariki.
Uliongea na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa zaidi ya mara 40 hiyo ni wastani wa karibia mara moja kila mwezi, ni wakati gani ulikuwa mzito zaidi kwako, kwa nini?

Kwa kweli kwanza niseme kwenye maisha yangu yote unaona Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwenye picha tu. Kwa hiyo kwanza nakumbuka siku ya kwanza...

Zaidi kuhusu mahojiano haya BOFYA HAPA