Timothy ageuza ukosefu wa ajira kuwa fursa ya biashara ya miwa Kenya
Timothy ageuza ukosefu wa ajira kuwa fursa ya biashara ya miwa Kenya
Leo tunammulika Timothy Henry, kijana huyu mkazi wa Embulbul Kaunti ya Kajiado nchini Kenya ambaye baada ya maisha ya ajira ‘kumtupa mkono’ aliamua kugeukia biashara ya juisi ya miwa na hivi sasa anashauri vijana wasisubiri ajira bali wajiajiri.
Ni dhahiri kuwa barani Afrika, vijana ndio idadi kubwa ya watu,na ukosefu wa ajira unaendelea kuwa changamoto kuu inayochochea umaskini, kinyume na lengo namba 1 la Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) la kutaka umaskini utokomezwe ifikapo 2030. Hata hivyo, baadhi ya vijana wanageuza changamoto hizi kuwa fursa.
Kipato cha kazi ya kufagia barabarani kikawa mtaji wa biashara ya sasa
Akiwa kwenye eneo la la biashara yake huko Embulbul, Timothy akizungumza na Redio Washirika Radio Domus, anasema alikuwa ameajiriwa kama fundi lakini ugonjwa wa coronavirus">COVID-19 ulisababisha kusimamishwa kazi. Baadaye aliingia kwenye kufagia barabara, kazi aliyofanya kwa mwaka mmoja.
Alipata jumla ya dola 500 na kisha akajiuliza afanye nini ili maisha yaendelee kusonga mbele? Ndipo akaingia kwenye uchuuzi wa juisi ya miwa. Alichagua biashara ya juisi ya miwa kwa kuwa miwa sio zao la msimu.
Miwa si zao la msimu, na si lazima uanze na mtaji mkubwa
“Mimi nimezaliwa kaunti ya Kisii ambako nafahamu sana zao la miwa. Lakini ukichukua zao la msimu, utapata shida. Lakini miwa hata nikienda Kisii sasa hivi nitapata miwa wakati wowote,” amesema Timothy ambaye anaongeza kuwa “nimekuzwa na miwa, hivyo ninaifahamu kwa kina.”
Sikiliza kwa kina hapa:
Tazama video hapa: