Ukweli kuhusu Malaria: WHO
Ukweli kuhusu Malaria: WHO
Afya
Haya ni mambo matano muhimu ya kuyafahamu kushuku ugonjwa wa Malaria duniani kwa mujibu wa Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO.
- Malaria bado ni tishio kubwa la afya duniani
Mwaka 2024, kulikuwa na wastani wa wagonjwa milioni 282 wa malaria na vifo 610,000 katika nchi 80 duniani kote. - Afrika ndiyo yenye mzigo mkubwa zaidi wa malaria
Kanda ya Afrika ya Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO, ilichangia asilimia 95 ya wagonjwa na vifo vya malaria duniani mwaka 2024, ikiwa na takribani ya wagonjwa milioni 265 na vifo 579,000. - Watoto wadogo ndio walio hatarini zaidi
Watoto walio na chini ya umri wa miaka mitano walichangia karibu asilimia 75 ya vifo vyote vya malaria barani Afrika 2024, hivyo kuwa kundi lililo katika hatari kubwa zaidi ya kuugua, kuathirika vibaya na kufariki dunia. - Malaria huenezwa na mbu lakini inaweza kuzuilika na kutibika
Malaria husababishwa na vimelea vya Plasmodium vinavyoenezwa kupitia kung’atwa na mbu wa kike aina ya Anopheles walioambukizwa. Ugonjwa huu unaweza kuzuiliwa kwa kutumia vyandarua, dawa za kufukuza mbu, tiba za kinga na chanjo. - Chanjo zinasaidia kupambana na malaria Afrika
Tangu mwaka 2021, WHO imependekeza matumizi ya chanjo za malaria kama RTS,S/AS01 na R21/Matrix-M kwa watoto wanaoishi katika maeneo yenye maambukizi makubwa. Chanjo hizi zinatarajiwa kuokoa makumi ya maelfu ya maisha ya watoto kila mwaka.