Nchi zinakuja Kenya kujifunza tunavyotekeleza vizuri SDGs - Hanna Wendot Cheptumo
Nchi zinakuja Kenya kujifunza tunavyotekeleza vizuri SDGs - Hanna Wendot Cheptumo
Wanawake
Imesalia miaka minne kufikia kilele cha miaka 15 ya utekelezaji wa Malengo 17 ya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo Endelevu, SDGs. Kuelekea mwaka 2030 mataifa yanaendelea kujitathimini ni kwa kiasi gani wanafanikiwa katika kuyatekeleza malengo hayo.
Kandoni mwa Mkutano wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake Duniani, CSW70 uliofanyika mwezi uliopita katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani, Anold Kayanda wa Idhaa hii aliketi na Hanna Wendot Cheptumo Waziri wa Jinsia, Utamaduni na Maslahi ya Watoto wa Jamhuri ya Kenya ili kusikia ni kwa namna gani Kenya inapiga hatua katika Lengo namba 5 la Usawa wa Kijinsia.