China na Urusi zapinga rasimu ya azimio ya kufanikisha safari mlango wa baharí wa Hormuz
China na Urusi zapinga rasimu ya azimio ya kufanikisha safari mlango wa baharí wa Hormuz
Rasimu ya Azimio iliyowasilishwa mbele ya wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa lengo la kuchagiza nchi zinazotumia mlango wa bahari wa Hormuz kuchangia katika kuhakikisha usalama wa meli zenye bidhaa za kibiashara zinazotumia mlango huo, imegonga mwamba baada ya Urusi na China kuipinga kwa kutumia kura turufu licha ya kura 11 za ndio.
Bahrain ndiyo iliyowasilisha rasimu hiyo iliyokuwa inaungwa mkono na nchi za Ghuba ambazo ni Kuwait, Qatar, Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu, (UAE) pamoja na Jordan.
Mchanganuo wa kura unaonesha kuwa wajumbe 11 walipiga kura za ndio ambao ni Bahrain, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, (DRC), Denmark, Ufaransa, Ugiriki, Latvia, Lberia, Panama, Somalia, Uingereza na Ufaransa.
Kura mbili za hapa ni kutoka Urusi na China ambazo zina kura turufa, ilhali wajumbe wawili amba oni Colombia na Pakistan hawakuonesha msimamo wowote.
Usalama unaozungumzwa ni pamoja na kusindikiza meli za biashara huku rasimu iliitaka Iran iache mara moja mashambulizi dhidi ya vyombo vya baharini vya kibiashara na jaribio lolote lile la kuzuia meli kupiga kambi kwa muda na vile vile kuacha kushambulia miundombinu ya kiraia, kama vile maji, mitambo ya kuondoa chumvi kwenye maji na mitambo ya mafuta na gesi.