Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ninasoma uadishi wa habari ili kufanikisha SDGs – Mkurugenzi wa ICCAO Tanzania

Mwanamke na mwanamume wanakaa kwenye viti vikubwa vikubwa vikubwa vinavyoangaliana wakati wa mahojiano katika studio moja wakiwa na nembo kubwa ya Umoja wa Mataifa kwenye skrini ya bluu nyuma yao.
UN News Zahra Salehe (kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la ICCAO katika mahojiano na Anold Kayanda wa Idhaa ya Umoja wa Mataifa Jijini New York, Marekani, Machi 2026.

Ninasoma uadishi wa habari ili kufanikisha SDGs – Mkurugenzi wa ICCAO Tanzania

Na Anold Kayanda
Malengo ya Maendeleo Endelevu

Ni desturi ya Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa kuwauliza baadhi ya washiriki wa mikutano inayofanyika katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani ni jambo gani wanakuwa wamejifunza katika mkutano husika na wataenda kulitekeleza katika nchi zao.

Mwaka jana 2025 katika mkutano wa 69 wa kamisheni ya hali ya wanawake duniani CSW69 mmoja wa waliohudhuria wakati huo ni Zahra Salehe, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la ICCAO linaloshughulika na masuala ya vijana nchini Tanzania na kuwa mwaka huu 2026 Zahra ameshiriki tena katika  mkutano wa 70 wa kamisheni ya hali ya wanawake duniani, CSW70, Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa imepata fursa ya kumuhoji ni kwa kiasi gani amefanikiwa katika kutekeleza malengo yake ya mwaka jana.
 
Pamoja na mafanikio mengine, katika mahojiano na Anold Kayanda wa Idhaa ya Umoja wa Mataifa Jijini New York, Marekani mnamo mwezi Machi 2026 Zahra Salehe anaeleza kuhusu uamuzi mpya aliouchukua wa kusomea taaluma ya uandishi wa habari katika shahada yake ya uzamivu ili kufanikisha Malengo ya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo Endelevu, SDGs.