Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zanzibar yaboresha huduma za mahakama kuvutiwa wanawake kusaka haki

Wanawake wawili wameketi kwenye meza ya mviringo yenye rangi ya bluu wakiwa na maikrofoni, wakirekodi podcast katika studio yenye alama ya Umoja wa Mataifa.
UN News Chausiku Fuya (kulia), Naibu mrajisi wa mahakama kuu Zanzibar katika mahojiano na Leah Mushi (kushoto) wa UN News Kiswahili kandoni mw amkutano wa CSW70.

Zanzibar yaboresha huduma za mahakama kuvutiwa wanawake kusaka haki

Na Leah Mushi
Wanawake

Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar nchini Tanzania imeeleza kupiga hatua katika kuweka mazingira rafiki kwa wanawake na watoto kwenda kusaka haki mahakamani. 

Akizungumza na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa Naibu Mrajisi wa Mahakama Kuu ya visiwani Zanzibar Chausiku Kafuti Kuya amesema sasa kuanzia miundombinu hadi huduma maalum kwa wanawake zinapatikana katika mahakama zote kuangia ngazi za wilaya. 

“Mahakama sasa ziko rafiki n miundombinu ni ya kisasa kabisa. Mwanamke shida yake kubwa alikuwa akijiuliza mimi nina mtoto nikienda mahakamani nitamuweka wapi? Hivi sasa kuna sehemu maalum ambao anaweza akaja pale akamyonyesha mtoto wake na baadaye akaingia kwenye mahakama akaendelea na na kesi. Kuna sehemu maalum ambayo tunaweza tukampatia mpaka huduma ya kwanza labda ikitokea kuna dharura tuna mazingira mazuri, lakini kama kwamba haitoshi kwa watoto sasa. Watoto wana mpaka sehemu za kucheza ambazo ni rafiki kabisa.” 

Moja ya changamoto kubwa visiwani Zanzibar ni masuala ya udhalilishaji watoto na kuingiliwa nalo pia naibu mrajisi wa mahakama amesema wamelishighulikia. 

“Mwaka 2021 kulianzishwa Mahakama Maalum za kushughulikia tatizo hilo na sasa hizi kesi hazichukui muda mrefu, zinasikilizwa kwa muda mfupi. Kwa sasa hivi kesi baada ya kwenda labda mwaka mmoja kesi itasikilizwa kwa miezi miwili mpaka miezi mitatu kumalizika kwa malalamiko ya kesi inachukua muda mrefu kumeisha kabisa. Haki inapatikana kwa wakati, lakini bila kuacha athari kubwa kwa mtu ambaye ametendewa kile kitendo cha udhalilishaji. Kwani kumkumbusha kila mara nako kumaleta Athari kwake. 

Kuhusu nafasi za uongozi katika mahakama 

Kuya amesesema kwa sasa hivi Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi Mahakamani ni mwanamke “lakini tuna mrajisi wa Mahakama pia ni mwanamke na hivi karibuni tu tumempata mwenyekiti mahakamani pia ni mwanamke na miummi naibu mrajisi pia ni mwanamke.:

Kwneye suala jingine la watoa hukumu za mashauri amesema nako idadi ya wanawake wameongezeka. “Tuna jumla ya majaji kumi na tatu Zanzibar katika majaji hao nane ni wanaume lakini watano ni wanawake.”

Mahakama ya Kadhi

Mfumo wa mahakama Zanzibar unapia mahakama ya kadhi ambayo inasikiliza mashauri kwa kufuata miongozi ya dini ya kiislamu. 

“Ujio wa sheria namba nane thelathini na tatu imekuja kutanua mawanda ya Mahakama ya Kadhi. Kuwepo kwa hii sheria kumetanua mawanda ya mahakama hii na sasa hivi imeruhusu wasuluhishi wanawake na wamepewa nafasi kubwa kabisa. 

Na je wananchi wamepokeaje suala hilo? “Wananchi wamepokea kwa uzuri kabisa kwa sababu unajua kuna masuala ya kike ambayo muda mwingine unajisikia ukizungumza na mwanamke mwenzio atakuelewa vizuri zaidi, lakini ana uhuru wa kuzungumza nao na wako mweingi. 

Mwanamke katika hijab ya bluu akizungumza kwenye kipaza sauti cha studio dhidi ya background ya bluu.
UN News Chausiku Fuya- Naibu mrajisi wa mahakama kuu Zanzibar katika mahojiano na Leah Mushi wa UN News Kiswahili kandoni mw amkutano wa CSW70.

Maboresha katika matumizi ya teknolojia

Mwandishi:Tunafahamu kwamba teknolojia inaendelea kukua na mahakama pia na zenyewe zinachukua mfumo wa teknolojia. Kuna lolote ambalo limefanyika Zanzibar. 

Kuya: Ndio, Mheshimiwa Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dokta Hussein Ali Mwinyi alizindua mfumo wa usikilizaji na ufunguaji mashauri, yaani Mfumo wa Kielektroniki wa Kufungua na kusikiliza mashauri. Mfumo huu kwanza unaruhusu kumsikiliza shahidi hata akiwa mbali. Sasa ule muda wa mtu kutoka sehemu mbali kuja kufuata mahakama kutoa ushahidi sasa hivi utakuwa umepungua. Ushahidi sehemu yoyote ambayo yuko yeye mwenyewe anaweza kuhudhuria kwenye zile sehemu ambazo zimepangwa na mahakama. Akaenda pale kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa kwa kuzifuata, halafu akaenda kutoa ushahidi wake sehemu yoyote ambayo karibu sasa hii inafanya kupunguza matumizi ya muda, lakini pia kipato yapo.

Mwandishi: Mfano, mtu moja yuko Mwanakwerekwe na mwingine labda yuko Paje, ana uwezo wa kwenda mahakama nyingine? 

Kuya: Ndio, anaweza kwenda kabisa kabisa, anaweza kwenda kwenye zile sehemu ambazo zimeelezwa kwenye kanuni akaunganishwa na akasikiliza kesi yake ikaendelea vizuri na ikamalizika vizuri bila shida yoyote. 

Mwandishi: Kama naibu mrajisi wa mahakama je ni changamoto zipi ambazo zinakufanya ushindwe kulala usiku? 

Kuya: Uelewa wa jamii kwa sababu tunaweza tukafanya yote haya, lakini jamii bila kuelewa hichi nitakipata wapi, nipite njia gani itakuwa bado kumaliza tatizo na hicho ndio kitu ambacho kina ninyima usingizi. Na nimesema nikitoka huku (Kwenye mkutano wa 70 wa CSW) hicho ndio kitu cha kwanza ambacho nitashughulika nacho. Ni kutengeneza mikakati ya kuwafikia wanajamii kwa wingi ili waelewe sasa wapite njia zipi ili wafikie kwenye mafanikio ambayo sisi mahakama tunatarajia kuyafikia.