Epusha ubaguzi dhidi ya watu wanaoishi na VVU - UNAIDS
Katika siku ya kimataifa ya kutokomeza ubaguzi tarehe Mosi Machi, Umoja wa Mataifa unaadhimisha haki ya kila mtu ya kuishi maisha kamili na yenye tija kwa utu. Mwaka huu, shirika la Umoja wa Mataifa la Kukabiliana na Ukimwi, UNAIDS linaangazia ubaguzi unaoendelea kukabili watu walioko hatarini kutokana na kuishi na Virusi Vya Ukimwi, VVU, ubaguzi unaodhoofisha upatikanaji wa huduma za afya, kuvunja haki, na kuzuia maendeleo ya kumaliza UKIMWI ifikapo 2030.
Kupitia wavuti wake, UNAIDS inasema maudhui ya siku hii ni binadamu kupatiwa umuhimu, au kupewa kipaumbele kwa muktadha wa unyanyapaa au ubaguzi dhidi ya watu wanaoishi na VVU.
Ushahidi ni wazi
Unyanyasaji na ubaguzi unaohusiana na VVU unaweka maisha hatarini. Kulingana na takwimu kutoka kwa watu zaidi ya 30,000 wanaoishi na VVU katika nchi 25, unyanyasaji na ubaguzi bado ni vikwazo vinavyoenea na kukwamisha upatikanaji wa huduma za afya, heshima, na haki za binadamu.
Ripoti halisi kuhusu watu wanaoishi na VVU na kukabiliwa na unyanyapaa inaonesha kuwa takriban 1 kati ya 4 anaripoti kufanyiwa unyanyasaji na wengine, ikiwemo katika huduma za afya, ambapo ubaguzi unadhoofisha imani na upatikanaji wa huduma za kuokoa maisha.
Zaidi ya hayo, asilimia 85 ya watu wanaoishi na VVU wanahisi unyanyapaa uliowekwa ndani yao, na wengi hubadilisha tabia zao — kuficha hali yao ya VVU au kusitisha matibabu ya VVU — kwa hofu ya kukataliwa na kuhukumiwa. Matokeo haya yanathibitisha kuwa unyanyasaji unaohusiana na VVU si suala dogo; ni kikwazo cha kumaliza UKIMWI ifikapo 2030.
Takwimu zinazungumza kuliko maneno |
|---|
|
Kwa wanawake na wasichana wanaoishi na kuathiriwa na VVU, ukosefu wa usawa wa kijinsia unachanganyika na unyanyasaji unaohusiana na VVU. Kubebeshwa ujauzito bila ridhaa, unyanyasaji na ukatili ni matukio yanayoendelea na yanayozidi kuenea ya unyanyasaji na ubaguzi yanayotokea ndani ya huduma za afya. Ukaguzi wa takwimu uliokusanywa kutoka kwa wanawake 26,502 wanaoishi na VVU kutoka nchi 23, ambao hivi karibuni ulikamilisha ulionesha kuwa katika kila nchi, wanawake wanaoishi na VVU wameripoti kupata aina fulani ya ukatili katika miezi 12 iliyopita.
Ubaguzi unaochanganyika na hali za kijinsia pia unaathiri vibaya uzoefu wao wa kupata huduma nyingine, maisha ya jamii na nyumbani, na upatikanaji wao wa haki na fidia. Zaidi ya hayo, unyanyasaji unaohusiana na VVU unachanganyika na kanuni na ukosefu wa usawa wa kijinsia kupeleka mzigo mkubwa wa huduma zisizotambuliwa na zisizolipwa kwa wanawake na wasichana.
Kinachopaswa kufanyika
Kuondoa sheria za kibaguzi
Nchi lazima zichambue sera na sheria zao na kuondoa zile zinazobagua, kuhalalisha na kudhuru watu wanaoishi na VVU — ikiwemo sheria zinazohalalisha biashara ya ngono, matumizi ya madawa, uhusiano wa jinsia moja, na kutofichua hali ya VVU — ambazo zinazuia upatikanaji wa huduma za afya.
Kulinda haki za kupata huduma za afya
Kuhakikisha usiri, kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wa afya na kutekeleza sera ya kutokuwa na uvumilivu kwa ubaguzi, kuondoa upimaji wa lazima wa VVU na kutoa huduma bora, zenye huruma kwa wote
Kushughulikia unyanyasaji katika jamii
Kupinga hadithi potofu na taarifa zisizo sahihi kuhusu VVU, kuelimisha umma kuhusu ukweli kwamba wenye VVU wanaotumia dawa ipasavyo hawaambukizi virusi kwa wengine (untransmittable).
Kuunga mkono hatua za jamii
Unga mkono hatua kama vile kupatia fedha mashirika yanayoongozwa na watu wanaoishi na VVU
Kushiriki ukweli
Tumia mitandao ya kijamii, maeneo ya kazi, na shule kusambaza ujumbe kuwa VVU ni hali ya kiafya, si dhambi, na kwamba watu wanaoishi na VVU wanaweza kuishi maisha marefu, yenye afya na heshima.