Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Barbara Batte Guevara na harakati za kueneza Kiswahili nchini Cuba

Kikundi cha watu, ikiwa ni pamoja na mwanamume aliyevaa mavazi ya Kiswahili ya jadi nyekundu akiwa ameshika fimbo, wakijipiga picha huko Havana, Cuba, wakati wa hafla ya elimu au utamaduni iliyozingatia lugha ya Kiswahili.
UN News
Barbara Batte Guevara (kulia) akiwa na wanafunzi wa lugha ya Kiswahili jijini Havana, Cuba.

Barbara Batte Guevara na harakati za kueneza Kiswahili nchini Cuba

Utamaduni na Elimu

Chuo Kikuu cha Havana nchini Cuba. Kwa kushirikiana na Tanzania chuo hicho ambacho mwezi uliopita kimetimiza miaka 298 tangu kuanzishwa kwake, hivi karibuni kimetoa fursa kwa Wacuba kujifunza lugha ya Kiswahili.

Darasa katika mji wa Havana, Cuba, ambapo wanafunzi wenye sare nyeupe na nyekundu wanajifunza Kiswahili, na mwalimu akiwasilisha kwenye skrini.
UN News

Ili kufahamu zaidi kuhusu hatua hii na mafanikio yaliyofikiwa hadi kufikia sasa, Anold Kayanda wa Idhaa ya Umoja wa Mataifa amemtembelea Profesa Barbara Batte, Mkufunzi anayefundisha lugha ya Kiswahili, yeye na wenzake katika Chuo Kikuu cha Havana na katika Nyumba ya Afrika nchini Cuba.

Kikundi cha wanafunzi wadogo na mtu mzima wameketi pamoja kwenye benchi la jiwe huko Havana, Cuba, wakifanya shughuli za kujifunza zinazohusiana na elimu ya lugha ya Kiswahili.
UN News

Takribani miaka 43 iliyopita, Barbara Batte Guevara, alijifunza kwa muda mfupi lugha ya Kiswahili nchini Tanzania lakini mbegu hiyo iliyopandwa karibia nusu karne iliyopita, anataka aipande kwa Wacuba wengine ili ichipue na kuzaa miche zaidi ya lugha ya Kiswahili kote Cuba, ukanda wa Karibiani na hata kote Amerika.