Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mchango wa Tanzania katika mkutano wa 64 wa Kamisheni ya UN ya Maendeleo ya Kijamii

Mwanadiplomasia wa Tanzania amevaa miwani, suti, na tai, akifanya ishara wakati akizungumza katika hafla ya Umoja wa Mataifa iliyozingatia SDGs na CSocD64.
UN News
Amon Mpanju, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumwa nchini Tanzania akizungumza na UN News Kiswahili kandoni mwa Mkutano wa UN CSocD64 kuhusu SDGs.

Mchango wa Tanzania katika mkutano wa 64 wa Kamisheni ya UN ya Maendeleo ya Kijamii

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Kikao cha 64 cha Kamisheni ya Maendeleo ya Kijamii (CSocD64) kilichoanza tarehe pili mwezi huu wa Februari hapa katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani kimehitimishwa leo Februari 10.

Kamisheni hii ni chombo cha ushauri kinachohusika na nguzo ya maendeleo ya kijamii kwa maendeleo ya kimataifa.

Anold Kayanda wa Idhaa ya Umoja wa Mataifa amezungumza na mmoja wa waliohudhuria mkutano wa mwaka huu akiwakilisha Tanzania; Amon Mpanju, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum na anaanza kwa kueleza zaidi kuhusu mkutano huu.