Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

YALIYOJIRI JARIDANI LEO:Mambo muhimu ya kuepuka saratani/Sudan Kusini njiapanda/Mifereji ya umwagiliaji Dodoma

Lucy Githinji amesimama karibu na gari la waridi na jeupe, akiwa ameshika bango linalosomeka 'Mimi ni Mwokozi wa Saratani ya Matiti kwa Miaka 3' wakati wa matembezi ya uhamasishaji wa saratani.
UN News/Assumpta Massoi Lucy Githinji, mkazi wa jimbo la New Jersey nchini Marekani katika matembezi ya hiari kwa ajili ya kuhamasisha jamii kuhusu saratani ya titi.

YALIYOJIRI JARIDANI LEO:Mambo muhimu ya kuepuka saratani/Sudan Kusini njiapanda/Mifereji ya umwagiliaji Dodoma

Amani na Usalama
  1. Mikakati mitatu ya WHO ya kutokomeza saratani
  2. Wananchi Sudan Kusini wako njiapanda kuamua wasonge mbele na amani au waendelee na machafuko.
  3. UNCDF yaleta matumaini kwa wakulima Dodoma, Tanzania kupitia mradi wa umwagiliaji

1.Fahamu mikakati 3 ya kuondokana na saratani

Shirika la Umoja wa Mataifa la afya duniani, wHO Kanda ya Afrika katika kupambana na saratani imekuja na mipango mitatu, wa kwanza ni mpango wa Dunia wa kutokomeza saratani ya shingo ya kizazi kwa sababu hii inaweza kutokomezwa kwa kufanya uchunguzi wa mapema kwa kutumia vifaa vya kisasa pamoja na kupima virusi vya HPV. Wa pili, ni mpango wa saratani kwa watoto unaoangazia maeneo makuu sita. Na mpango wa tatu ni mpango wa saratani ya titi kwa kuwa hii ndio inayoongoza katika nchi za Afrika zilizo kusini mwa jangwa la Sahara.
 
Mikakati hii imetajwa wakati ambapo Daktari Dillé Issimouha Mahamadou, mshauri wa masuala ya Saratani katika shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani (WHO) Kanda ya Afrika  anaeleza kuwa mambo yanayohusiana moja na moja na kuleta ugonjwa wa saratani ni pamoja na unywaji wa pombe kupindukia na uvutaji wa sigara.
 
Anasema, “kuna virusi kama vya Human Papilloma Virus, (HPV) vinavyosababisha saratani,  na ugonjwa wa homa ya ini aina ya B ambao nao pia unaweza kusababisha saratani ya shingo ya kizazi. Pombe inaweza kusababisha saratani ya titi. Na kitu kikubwa watu wasichokijua ni kwamba, hata kuishi kwenye mazingira ambapo kuna uvutaji wa sigara kunaweza kukuweka katika hatari kubwa ya kupata ugonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi.”
Kikundi cha watu kwenye tamasha la ndani huko Sudan Kusini, wakionyesha ufundi wa jadi na kukuza amani na biashara chini ya bendera ya UNMISS.
UNMISS Washiriki wa jumuiya katika tamasha la ndani linaloungwa mkono na UNMISS nchini Sudan Kusini, wakisherehekea amani na biashara kupitia sanaa za kitamaduni.

2. Sudan Kusini iko nijia panda na wananchi wanalitambua hilo: UNMISS

Sudan Kusini iko katika njia panda na wakati muhimu sana baada ya miaka ya migogoro, taifa changa zaidi duniani linakabiliwa na chaguo gumu, kurejea katika vurugu kubwa za maafa, au kusonga mbele kuelekea amani. Mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo UNMISS unasema wananchi wana sauti ya kudhihirisha mwelekeo.
 
Mjini Mangalla wakati viongozi wa kisiasa wakiendelea kugawanyika, katika mji huu mdogo wa jimbo la Equatoria ya Kati, wananchi wa kawaida wanachagua njia tofauti. Hapa, familia kutoka pembe zote za nchi wanaishi pamoja. Zaidi ya makabila sitini na nne huita Mangalla nyumbani. Licha ya hofu, ugumu wa maisha na hali ya kutokuwa na uhakika, wakazi wanaamua kuzungumza badala ya kupigana.
 
Katika mazungumzo hayo ya kijamii yanayoungwa mkono na UNMISS, wanawake wako mstari wa mbele kuhimiza amani. Najwa Suleiman kiongozi wa wanawake ni miongoni mwao anasema, “tujiepushe na siasa. Tukianza kusikiliza wanaume na kutenda maneno yao, tutaiharibu nchi yetu. Sisi wanawake hatuna tatizo lolote kati yetu. Tatizo liko kwa wanaume wanaosambaza kauli za chuki miongoni mwa watu.”
 
Beneficiaries of irrigation project in Dodoma Region, Tanzania, inspecting the irrigation canals. The project has been successfully implemented by the United Nations Capital Development Fund (UNCDF) in collaboration with its partners, including the Government of Tanzania.
UNCDF Wanufaika wa mradi wa umwagiliaji mkoani Dodoma nchini Tanzania wakikagua mifereji ya umwagiliaji. Mradi hu umefanikishwa na Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya Mitaji UNCDF kwa ushirikiano na wadau wake ikiwemo serikali ya Tanzania.

 

3. UNCDF: Uwekezaji bunifu wasaidia wakulima Dodoma, Tanzania

Ukame ulipokumba Kijiji cha Kitati mkoani Dodoma mji mkuu wa Tanzania, Hadija Hussein mwenye umri wa miaka 70 alilazimika kuuza mifugo yake yote ili aweze kuishi. Kama wakulima wengine, hivi sasa amegubikwa na hofu kuwa pengine ukame kama huo unaweza kuibuka tena, lakini ndipo Umoja wa Mataifa ukachukua hatua kuondoa hofu hiyo. 

Bi. Hadija Hussein akiwa ameketi nyumbani kwake akikumbuka ukame uliomlazimu kuuza mali zake anasema nilijihisi vibaya sana katika hali ile, nilisalia bila kufahamu la kufanya. 

Hofu yake hiyo ilipatiwa jawabu na Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya Mitaji, UNCDF, ambao unasaidia wanaokumbwa na madhara ya mabadiliko ya tabianchi kujijenga mnepo ili changamoto hizo zinapotokea waweze kuhimili na kuendelea na maisha.

Video ya UNCDF inatupitisha kwenye shamba moja hapa Kitati wilayani Mpwapwa, moja ya wilaya za mkoa wa Dodoma, kwa uwezeshaji wa UNCDF miundombinu ya umwagiliaji ikiwa imejengwa na mifereji iko bayana kuelekeza maji kwenye mashamba. 

Bofya hapo chini kusikiliza taarifa nzima. 

Audio file