Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatua ya Marekani kujiondoa kwenye mashirika ya UN yamaanisha nini kwa tabianchi, biashara na maendeleo?

Kaunti ya Turkana, kaskazini mwa Kenya, hukumbwa na ukame mara kwa mara.
© UNCCD/Mwangi Kirubi Kaunti ya Turkana, kaskazini mwa Kenya, hukumbwa na ukame mara kwa mara.

Hatua ya Marekani kujiondoa kwenye mashirika ya UN yamaanisha nini kwa tabianchi, biashara na maendeleo?

Masuala ya UM

Mashirika na vyombo husika ni pamoja na:

  • UNFPA, UNCTAD, ITC na ICTRs, UN Women
  • Mikataba ya kimataifa ukiwemo UNFCCC wa mabadiliko ya tabianchi
  • Na baasdhi ya Ofisi za Wawakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa UN

Hatua ya wiki hii ya Marekani ya kutangaza kujiondoa katika vyombo kadhaa vya Umoja wa Mataifa inalenga miradi na mipango inayojikita katika maeneo kadhaa lukuki, ikiwemo janga la tabianchi, biashara, jinsia na maendeleo.

Pindi msemaji wa Umoja wa Mataifa Stéphane alipozungumza na waandishi wa habari Alhamisi jijini New York, Marekani kufuatia tangazo la Marekani, alisisitiza kuwa Shirika litaendelea kutelekeza majukumu yake kwa azma ile ile.

Tangazo la Jumatano la Marekani linaeleza kuwa serikali ya Marekani “inasitisha ushiriki wake katika au ufadhili kwenye vyombo hivyo kwa kadri inavyoruhusiwa kisheria.”

Vyombo kadhaa vilivyoorodheshwa kwenye taarifa hiyo hufadhiliwa kimsingi au kiasi kwa bajeti ya kawaida ya Umoja wa Mataifa, ikimaanisha kwamba ufadhili utaguswa na tangazo hilo la Marekani, ijapokuwa ufadhili mkuu utaendelea.

Hata hivyo, Ikulu ya Marekani inaeleza kuwa tathmini yake ya ufadhili kwa mashirika ya kimataifa inaendelea na kwa sasa haiku dhahiri madhara ya tangazo la sasa yatakuwa ni kwa kiasi gani.

Hapa tunakuwekea bayana mchanganuo wa vyombo 31 vya Umoja wa Mataifa vilivyotajwa kwenye tangazo hilo la Marekani, na mchango wa vyombo hivyo katika maisha ya watu, jamii na mataifa kwa ujumla.

Masula ya Afrika

Washiriki katika Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Hali ya Hewa wanatoa wito wa ufadhili zaidi ili nchi ziweze kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
© UNFCCC/Zô Guimarães

Tabianchi na Mazingira

Uratibu

Maendeleo

Vyoo vipya katika shule ya msingi ya Lubile iliyoko jimbo la Tanganyika nchini Jamhuri ya Kidemorkrasia ya Congo, DRC. Vyoo hivi vimejengwa kwa msaada wa UNICEF na Education Cannot Wait.
© UNICEF/Josue Mulala

Elimu na Mafunzo

  • Chuo cha UN cha Mafunzo na Utafiti (UNITAR): Hutoa mafunzo na kujengea uwezo watu mmoja mmoja, mashirika nan chi, (hususan mataifa yanayoendelea) kwenye maeneo kama vile diplomasia, maendeleo endelevu, mabadiliko ya tabianchi na usimamizi wa majanga
  • Chuo cha UN cha Mafunzo kwa Watumishi: Hupatia watumishi wa UN mafunzo, na huduma za ushauri ili kuhakikisha nguvu kazi ina uwezo, inaendana na mazingira na inafanya kazi kwa ushirikiano
  • Chuo Kikuu cha UN: Tanuru la fikra la UN na hutoa mafunzo ya shahada za juu, hufanya tafiti na hutoa miongozo ya kisera kwenye masuala muhimu ya dunia
  • Education Cannot Wait: Mfuko wa Umoja wa Mataifa uliojikita katika kufadhili elimu kwenye maeneo yenye dharura na majanga yaliyodumu muda mrefu, ili kuhakikisha watoto na vijana walioathiriwa vibaya na majanga, ukimbizi na wanapata elimu bora na kwa usalama

Jinsia

Muuguzi katika chumba cha kupanga familia huko Centro de Saúde do Ramiro, Luanda, Angola, anawaeleza wanawake wawili vijana njia za kuzuia mimba.
© UNFPA/Noriko Hayashi

Afya

  • NShirika la UN la Idadi ya Watu (UNFPA) : Husongesha afya na haki za uzazi kwa wote, na kukuza usawa wa kijinsia na hukusanya takwimu za idadi ya watu kwa ajili ya maendeleo, ikisaidia kupunguza vifo vya akina mama na kupanua upatikanaji wa huduma za uzazi wa mpango.

Sheria ya Kimataifa

  • Kamisheni ya Kimataifa ya Sheria: Husimamia uendelezaji na urasimishaji wa sheria za kimataifa kwa kuandaa vyombo vya kisheria na kufafanua kanuni; kukuza utawala wa sheria, na kuunga mkono mahusiano ya amani baina ya mataifa.
  • Mfumo wa Kimataifa wa Masalia ya Mahakama za Kimataifa za Uhalifu : Hutekeleza majukumu muhimu ya Mahakama za Kimataifa za zamani za makosa ya  uhalifu za Rwanda na Yugoslavia, hukamilisha kesi zinazoendelea, hulinda mashahidi na kuhifadhi kumbukumbu, kuhakikisha uwajibikaji kwa uhalifu mkubwa wa kimataifa.

Kupunguza mizozo na ghasia

Kitengo cha tabia na nidhamu cha MONUSCO kinasaidia manusura wa ukatili na unyanyasaji wa kingono eneo la Sake jimboni Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kama sehemu ya ujenzi wa amani kwenye eneo hilo lililokumbwa na machafuko.
MONUSCO

Biashara na Uchumi