Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vijana wabadilisha kilimo na maisha yao kupitia mradi wa EKYAN

UNICEF Kenya imeunga mkono mradi wa vijana uitwao Empowering Kenyan Youth in Agribusiness and Nutrition (EKYAN) kuwawezesha vijana kwa mafunzo ya kilimo rejelevu.
© UNICEF
UNICEF Kenya imeunga mkono mradi wa vijana uitwao Empowering Kenyan Youth in Agribusiness and Nutrition (EKYAN) kuwawezesha vijana kwa mafunzo ya kilimo rejelevu.

Vijana wabadilisha kilimo na maisha yao kupitia mradi wa EKYAN

Ukuaji wa Kiuchumi

Kutoka mashambani hadi kwenye majukwaa ya kidijitali, vijana wa kaunti ya Kirinyaga nchini Kenya wanaongoza enzi mpya ya kilimo kinachoendana na mabadiliko ya tabianchi. Shirika la Umoja wa Mataifa la Watoto (UNICEF)  limeunga mradi wa vijana uitwao Empowering Kenyan Youth in Agribusiness and Nutrition (EKYAN) kuwawezesha vijana kwa mafunzo ya vitendo na zana muhimu ili kukuza biashara zao za kilimo, kuimarisha mifumo ya chakula ya ndani, na kujenga jamii zinazoimili mabadiliko ya tabianchi.

Mradi wa EKYAN inalenga kufikia na kuwawezesha vijana 5,000 wajasiriamali wa kilimo, kufunza vijana 10,000 kuhusu mifumo endelevu ya chakula, na kuwafikia zaidi ya wakulima 60,000 kwa mbinu za kilimo kinachostahimili mabadiliko ya tabianchi ifikapo mwisho wa 2025.

UNICEF Kenya has supported a youth project called Empowering Kenyan Youth in Agribusiness and Nutrition (EKYAN) to empower youth with training in sustainable agriculture.
© UNICEF
UNICEF Kenya has supported a youth project called Empowering Kenyan Youth in Agribusiness and Nutrition (EKYAN) to empower youth with training in sustainable agriculture.

Kupitia mpango huu, vijana wanageuza ujuzi wao kuwa biashara bunifu za kilimo zinazostahimili mabadiliko ya tabianchi, huku wakiongeza fursa za kipato, kuimarisha mifumo ya chakula na kuboresha lishe. Felista Mutungi, mjasiriamali wa kilimo kutoka Kaunti ya Kirinyaga, anasema:  

Mpango wa EKYAN umekuza sana ujuzi wangu. Kabla ya mpango huu, tulikuwa tukilima mpunga kwenye robo ekari na kupata magunia manne hadi matano tu. Sasa, katika nafasi hiyo  ya robo ekari, tunaweza kuvuna hadi magunia saba.Hakika, kama si kwa msaada wa UNICEF na mpango wa kuwashirikisha vijana wa Kenya katika kilimo, sisingefikia mafanikio niliyoyapata leo.”

Eric Munene, anaeleza jinsi kilimo kimekuwa msingi wa mafanikio yake ya kiuchumi na kubadili maisha yake kwa kiasi kikubwa.

Kilimo kimenisaidia kujenga nyumba. Nimenunua pikipiki. Faida niliyoipata baada ya kuuza mboga na nyanya imenifanya niweze kununua kuku 10, ng’ombe wawili na mbuzi wawili. Kilimo kimenisaidia kukua kimaakili.”

Eric Munene akiwa kwa shamba lake. UNICEF Kenya imeunga mkono mradi wa vijana uitwao Empowering Kenyan Youth in Agribusiness and Nutrition (EKYAN) kuwawezesha vijana kwa mafunzo ya kilimo rejelevu.
© UNICEF
Eric Munene akiwa kwa shamba lake. UNICEF Kenya imeunga mkono mradi wa vijana uitwao Empowering Kenyan Youth in Agribusiness and Nutrition (EKYAN) kuwawezesha vijana kwa mafunzo ya kilimo rejelevu.

Kwa kutumia mifumo ya kidijitali, mbinu za kilimo kinachoendana na mabadiliko ya tabianchi na mitandao thabiti ya ushirikiano, EKYAN linawezesha kilimo kuwa chanzo cha ubunifu na fursa kwa vijana. Grace Nyawira, mjasiriamali wa kilimo kutoka Kirinyaga, ni miongoni mwa vijana wanaoendeleza mabadiliko haya kupitia mafunzo ya kilimo endelevu na lishe katika jamii. Anasema:

“Nimekuwa nikiwaelimisha wakulima kuhusu kilimo rejelevu na masuala ya lishe. Leo nitakutana na kikundi cha wakulima ambapo nilipanga kuwafundisha mbinu za kilimo rejelevu. Vikundi vitatu vya wakulima ni vya wanawake, na pia huwa nawafundisha wanafunzi takribani wanafunzi 50 kutoka shule ya msingi niliyoambatanishwa nayo.

Kujifunza hadi kujipatia riziki. Mafunzo kwa ajili ya mabadiliko. EKYAN ni modeli inayoweza kupanuliwa na kurudiwa kwa ujasiriamali wa kilimo unaoongozwa na vijana, mabadiliko ya lishe na uimarishaji wa mifumo ya chakula. Kufikia 2028, inalenga kuwawezesha wakulima milioni 2 kuboresha maisha yao.