Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afrika inataka nini katika COP30

Dkt. Richard Muyungi, Mjumbe Maalum wa Mabadiliko ya Tabianchi kutoka Tanzania, ameketi kwenye meza ya mkutano akiwa na bango la 'JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA' wakati wa mkutano wa kilele wa COP30 huko Belem, Brazil.
UN News Dkt. Richard Muyungi Mjumbe maalumu kwenye masuala ya mabadiliko ya tabianchi na mazingira kutoka nchini Tanzania.

Afrika inataka nini katika COP30

Tabianchi na mazingira

Katika mkutano wa Nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi COP30 unaendelea huko mjini Belém, Brazil bara la Afrika linasema huu ni wakati wa utumizaji wa ahadi za kifedha zilizoahidiwa mwa muda mrefu ili kuweza kuhakikisha mapambano ya athari za mabadiliko ya tabianchi yanakamilika huku kukiwa na uhamaji wenye haki kutoka nishati isiyo jadidifu Kwenda nishati safi.

Dkt. Richard Muyungi mjumbe maalumu kwenye masuala ya mabadiliko ya tabianchi na mazingira kutoka nchini Tanzania ambaye pia ni mwenyekiti wa nchi za Afrika, kwa maana ya kwamba wataalamu na mabalozi wanaosimamia masuala ya mabadiliko ya Tabianchi katika nchi zao Kundi lilioanza mwaka 995 ambapo mwaka huu wanatimiza miaka 30.

Swali: Ukiwa mwenyekiti unayewakilisha bara lenye nchi zaidi ya 50 zinazotofautiana kuikubwa na kijiografia ambapo kuna nchi zenye miti na Bahari, nyingize hazina na hata visiwa vidogo, unahakikisha vipi kuwa masuala ya kila nchi yanayohusiana na mabadiliko ya tabianchi wanawakilishwa ipasavyo?

Wanaharakati wa hali ya hewa wana mabango na bango kubwa lililoandikwa 'FEDHA ZA MAKUBALIANO SASA' wakati wa maandamano katika COP30 huko Belém.
© UNFCCC/Zô Guimarães Washiriki katika Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Hali ya Hewa wanatoa wito wa ufadhili zaidi ili nchi ziweze kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Jibu: Kama mwenyekiti ninachofanya kwanza nikusema kwa niaba ya Afrika ina maana agenda zote za bara mimi ndio nazisimamia. Tunazo ajenga kuu muhimu tano ambazo ndio zimetuleta (Belém, Brazi), kuna ajenda kubwa ya masuala ya fecha na katika hiki tulichokuwa tukiangalia ni maeneo matatu eneo moja kubwa ni masuala ya fedha.

  1. Fedha kwa ajili ya ahadi iliyotolewa katika COP29 – ni jinsi gani nchi zitapata fedha zinazojitosheleza kwa ajili ya mahitaji yake. Na hii tulikubaliana ifikapo mwaka 2035 nchi zitaanza kupata takriban dola trilioni 1.3 kwa ajili ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi lakini wakati huo huo tulikubaliana nchi zitatoa takribani dola bilioni 300 kila mwaka kwa ajili ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Agenda hii imekamilika na kwasasa tunaangalia ni jinsi gani tutakuwa na mpango kazi wa miaka ijayo.
  2. Agenda nyingine ni kuangalia jinsi gani tutaweka fedha za kutosha katika mifuko na kuhakikisha mifuko inaanza kufanya kazi. Kuna mfuko ulioanzishwa kwa ajili ya kuzisaidia nchi zetu kupambana na majanga loss and damage fund. Mfuko huu tayari umeshafanikiwa na tumeuzindua hapa kwenye COP30 na tayari kuanzia tarehe 15 Novemba nchi zitaanza kupata fedha kutoka mfuko huu. Kutakuwa na dirisha la takribani miezi sita kwa ajili ya nchi kuleta maombi ya kupata fedha na baadae nchi zitaruhusiwa kupata takriban dola milioni 5 hadi dola milioni 20 kwa kila mradi kwa ajili ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Hii tayari ni mafanikio ambayo tumeyapata katika wiki ya kwanza.
  3. Eneo jingine ambalo bado halijakamilika ni kuongeza fecha kwa ajili ya mahitaji. Katika mkutano wa BAKU sisi kama Afrika tulitaka tupate fedha takriban dola trilioni 3 kila mwaka lakini tukaishia kupata dola bilioni 300 na tukaweka mkakati wa kupata dola trilioni1.5. Tunachosema ni kuwa kuna mifuko inatakiwa kuwekewa fedha ambayo kwa sasa haina fedha za kutosha kulingana na changamoto zilizopo.

Kuhama kwa haki Kwenda kwenye matumizi ya nishati safi

Mwenyekiti huyo wa Afrika ametaja jambo lingine wanalo lizungumzia ambalo ni muhimu ni kuhama kutoka matumizi ya nishati zisizo jadidifu kwenda kwenye nishaji safi zitakazo saidia kupunguza gesi joto.

Dkt. Muyungi amesema “hili limekuwa jambo muhimu tunaloliangalia ni kwa jinsi gani litakuwa na faidi kwa nchi za Afrika na kugusa masuala muhimu kama vile kuhakikisha nchi za Afrika zinakuwa na umeme wa kutosha, pili ajenda ya nishati safi ya kupikia ipo kwenye mazungumzo ya uhamaji wa haki just transitions. Na tatu ni kuhakikisha inatoa fursa kwa vijana kupata ajira na kutumia rasilimali za afrika vyema kututoa tulipo hasa kwakutumia madini muhimu.”

Mvulana mdogo akiongoza kundi la ngamia hadi kwenye kingo ya maji katika eneo la Somalia nchini Ethiopia.
© UNICEF/Mulugeta Ayene Mvulana akiwasili kwenye chanzo cha maji katika eneo la Somalia nchini Ethiopia.

Kuhimili mabadiliko ya tabianchi

Suala jingine ambalo linajadiliwa kwenye mkutano huo wa mabadiliko ya tabianchi ambalo pia ni agenda ya bara la Afrika ni jinsi bara hilo linavyo jitahidi kuhimili mabadiliko ya tabianchi. Kwa takriban miaka miwili wataalamu wamekuwa wakijadiliana kuhusu viashiria vinavyoonesha kuna mabadiliko ya tabianchi. Huo ni mjadala mkubwa na mpaka sasa majadiliano ynaendelea na hawajafikia mwisho na hawajakubaliana na Dkt. Muyungi anaamini kuwa “kabla hatujafikia mwisho wa mkutano huu tutakuwa tumekubaliana na tumelikamilisha.”

Wito wa Afrika kwa dunia

Mwenyekiti huyo wa Afrika katika COP ameeleza kuwa namatarajio makubwa na mikutano hiyo huku akieleza kuamini kuwa dunia nzima huu ni mkutano muhimu sana. “wito kwa kudia ni kwamba tuhakikishe COP30 uwe ni utekelezaji sio maneno tu. Upatikanaji wa fedha kama tulivyo ahidiwa, utekelezaji wa viashiria vya kuhakikisha tunakabiana na badiliko ya tabianchi pamoja na kuhakikisha teknolojia tunazipata kama tunavyo zihitaji.” Amesem Dkt. Muyungi

Ameeleza matarajio yake ni kuwa mpaka wanahitimisha mkutano huu tarehe 21 Novemba 2025 basi watakuwa wanaondoka na maazimio ambayo ni ya utekelezaji zaidi badala ya kuwa na maazimio ambayo yanawarudisha nyuma kwa maana ya mazungumzo tu ambayo wamekuwa nayo kila mara.