Marekani yajinasibu kwa mafanikio ya kumaliza migogoro isiyokwisha
Marekani yajinasibu kwa mafanikio ya kumaliza migogoro isiyokwisha
Rais wa Marekani – Donald J. Trump akihutubia Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kikao cha 80 hii leo jijini New York amejinasibu kwamba amefanikiwa kumaliza mogogoro siyokwisha “Katika kipindi cha miezi saba, nimemaliza vita saba ambavyo havikuisha “amedai Rais huyo.
Hata hivyo, amesema Umoja wa Mataifa ulitoa msaada mdogo, huku akiuliza: “Nini maana ya Umoja wa Mataifa? Inaonekana wanaandika barua zenye maneno makali lakini maneno matupu hayawezi kumaliza vita.”
Tuzo kubwa ni kuokoa maisha ya mamilioni
Akiendelea kujinadi amesema wakati baadhi ya watu wanasema anapaswa kupewa Tuzo ya Amani ya Nobel, Trump amesema kwake “Tuzo halisi itakuwa kuokoa maisha ya mamilioni.”
Kuhusu Iran, aliyoiita “mwanaharakati nambari moja wa kigaidi duniani”, amesema kuwa uwezo wa taifa hilo wa kuongeza uzalishaji wa madini ya urani “ulisambaratishwa kabisa, na utawala wake pia uliongoza kumaliza vita vya siku 12.”
Kuhusu Ukraine, amekiri kwamba “nilidhani kwamba hivyo vitakuwa vita rahisi kumaliza” kutokana na uhusiano wake na Rais wa Shirikisho la Urusi Vladimir Putin.
Badala yake, amesema mgogoro umeendelea kwa miaka mitatu, “ukiua vijana elfu tano hadi saba kila wiki.”
Amezilaumu nchi za muungano wa NATO kwa unafiki akisema ni “Wanunua mafuta na gesi kutoka Urusi wakati wanaposema wanashughulika nasuala la Urusi,”. Suluhisho lake lililopendekezwa ni ushuru, amesema “Ikiwa Urusi haitamaliza vita, Marekani itaweka ushuru mkali sana ambao ungemaliza vita haraka, lakini watu wa Muungano wa Ulaya wanapaswa pia kuutekeleza.”
Ametoa wito wa hatua za haraka kuchukuliwa Gaza kufuatia hali mbayá ya kibinadamu lakini pia kuachiliwa kwa mateka wote, na ameonya kuwa kutambuliwa tu kwa taifa la Palestina itakuwa ni “zawadi kwa Hamas kwa ukatili wake mbaya.”
Ukraine: India na China zinafadhili vita
Akizungumzia uvamizi wa Urusi kwa Ukraine kwa kiwango kikubwa, Trump amezishutumu India na China kwa kufadhili vita kwa kununua mafuta kutoka Urusi.
Trump pia aliikosoa nchi za Ulaya kwa kununua mafuta ya Urusi huku zikijaribu kuongeza shinikizo kwa Urusi.
Gaza: Utambuzi wa Palestina ni zawadi kwa Hamas
Ametoa wito wa hatua za haraka kuchukuliwa Gaza, kuachiliwa kwa mateka wote, na ameonya kuwa kutambuliwa pekee kwa taifa la Palestina kungekuwa ni “zawadi kwa Hamas kwa ukatili wake mbaya.”
Trump alisema kuwa uamuzi wa baadhi ya nchi kutambua taifa la Palestina utakuwa ni zawadi kwa Hamas.
Aliishutumu Hamas kwa kukataa kuwaachia mateka na kukataa "mapendekezo ya amani yenye mantiki. Hatupaswi kusahau Oktoba 7," amesema na kutoa wito wa kuachiliwa kwa mateka wote.
Uhamiaji: Ulaya inaharibiwa kwa sababu ya usalama wa kisiasa
Trump ametumia sehemu kubwa ya hotuba yake kuzungumzia uhamiaji. Kwa mujibu wake, mamlaka ya Marekani imechukua hatua madhubuti kudhibiti uhamiaji haramu.
Miongoni mwa hatua hizo ni kukamatwa kwa wingi na kufukuzwa kwa wale waliovuka mipaka kuingia Marekani kinyume cha sheria.
"Wamesimamisha kuja hapa. Hawaji tena," amesema Rais wa Marekani.
Kwa mujibu wake, hatua hizi pia zimesaidia kuokoa maisha ya wahamiaji wenyewe, kwani walikuwa wanapoteza maisha wakiwa safarini kuja Marekani.
Wakati huohuo, Trump ameushutumu Umoja wa Mataifa kwa kufadhili uhamiaji haramu, na pia kusema kuwa nchi za Ulaya zinaharibiwa kutokana na "uvamizi wa wahamiaji haramu. “
Ameongeza kuwa Ulaya haifanyi jitihada za kupunguza uhamiaji, na sababu ya hali hiyo ni "usalama wa kisiasa."
Tabianchi: Makadirio ya UN yalikuwa mabaya
Katika hotuba yake, Trump ameyaita mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabianchi kuwa ni "utapeli na kukosoa jitihada za nchi kupunguza utoaji wa hewa chafuzi”.
Amesema nishati mbadala au jadidifu ni ghali na haina ufanisi. Ameunga mkono matumizi ya makaa ya mawe, mafuta na gesi.
Trump pia amesema makadirio ya Umoja wa Mataifa na makundi mengine yanayopambana na mabadiliko ya tabianchi yalikuwa mabaya.
Utozaji ushuru ni mfumo wa kujilinda
Rais huyo wa Marekani amesema uamuzi wa serikali yake kutoza ushuru kwa nchi nyingi ni njia ya kulinda uchumi wa Marekani, ambao umedhurika kutokana na hatua za mataifa mengine yanayopuuza, kwa mujibu wake, kanuni za biashara ya kimataifa.
"Tunatumia ushuru kama mfumo wa kujilinda," amesema. Akiongeza kuwa uchumi wa nchi zilizozingatia kanuni uliteketezwa.