Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Brazil: Umaskini ni adui wa demokrasia kama vile ulivyo ugaidi 

Rais Luiz Inacio Lula da Silva wa Brazil akihutubia mjadala mkuu wa kikao cha 80 cha Baraza Kuu.
UN Photo/Loey Felipe
Rais Luiz Inacio Lula da Silva wa Brazil akihutubia mjadala mkuu wa kikao cha 80 cha Baraza Kuu.

Brazil: Umaskini ni adui wa demokrasia kama vile ulivyo ugaidi 

Amani na Usalama

Vita pekee ambayo kila mtu anaweza kushinda ni ile tunayopigania dhidi ya njaa na umaskini amesema Rais wa Brazil Luiz Inácio Lula Da Silva, akihutubia leo Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Jijini New York.

Rais huyo amewaambia nchi wanachama 193 kuwa Brazil imeondolewa kwenye ramani ya njaa ya Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa FAO mwaka huu 2025 ingawa duniani kote, watu bilioni 2.3 wanakabiliwa na ukosefu wa chakula.

Silaha isiwe kipaumbele cha dunia

Rais huyo wa Brazil akageukia vipaumbele vya jumuiya ya kimataifa akisistiza “ni lazima vigeukie kupunguza matumizi ya silaha, kuongeza misaada ya maendeleo, kupunguza madeni kwa nchi maskini zaidi na kuweka ushuru wa chini duniani ili matajiri wengi walipe ushuru zaidi kuliko wafanyakazi”.

Pia amesema ni lazima kudhibiti mtandao, jambo ambalo halimaanishi kupunguza uhuru wa maoni, bali kuhakikisha kuwa kile kilicho “haramu katika dunia halisi kinatendewa vivyo hivyo katika mazingira ya mtandao”.

Uhalifu lazima udhibitiwe

Rais Lula Da Silva amesisitiza kuwa upinzani dhidi ya udhibiti  wa mitandao unaficha uhalifu kama vile biashara haramu ya binadamu na unyanyasaji wa watoto.

Amekumbusha kuwa “Bunge la Brazil lilikuwa sahihi kuchukua hatua haraka kushughulikia suala hili” katika sheria mpya zilizopitishwa hivi karibuni.

Hakuna nguvu itakayoshinda ngumu ya Brazil

Rais Luiz Inácio Lula Da Silva, akizungumzia demokrasia duniani na nchini mwake amesema “Demokrasia na uhuru wetu havina mipaka ya majadiliano.” 

Kiongozi wa zamani wa Taifa alihukumiwa kwa mara ya kwanza kwa kushambulia demokrasia katika historia ya Brazil ya miaka 525, amesema.

Haki ya kujitetea mahakamani iliheshimiwa jambo ambalo lingewekezwa kizuizini chini ya udikteta.

Hii ilituma ujumbe kwa “wazushi wa udikteta na wafuasi wao kuwa demokrasia ya Brazil haiwezi kujadiliwa.”

Amesisitiza kuwa Brazil imekuwa na itaendelea kujitetea dhidi ya hatua za pande moja zinazolenga mahakama na uchumi wake.

Akielekeza kisa Amerika ya Kusini na Caribbea, amesema “Njia ya mazungumzo haipaswi kufungwa Venezuela. Haiti ina haki ya mustakabali bila ukatili. Na haiwezi kukubalika kwamba Cuba iorodheshwe kama nchi inayounga mkono ugaidi.”

Ametoa wito wa changamoto hizo kubwa za kimataifa kushughulikiwa kwa mshikamano na kutoruhusu mataifa machache kuingilia au kuvuruga demokrasia ya mataifa mengine.

Hali ya Gaza haikubaliki

Kuhusu vita inayoendelea Gaza na mauaji ya raia Rais huyo amesema  “Hapo, sheria ya kibinadamu ya kimataifa na dhana ya kipekee ya kimaadili ya Magharibi pia imezikwa. Mauaji haya yasingetokea bila ushirikiano wa wale ambao wangeweza kuyazuia.”

Alisema, “Ni jambo la kusikitisha kwamba Rais Mahmoud Abbas alizuiawa na nchi mwenyeji kushiriki katika dawati la Palestina katika wakati huu wa kihistoria.”

Kisha akagusia mabadiliko ya tabianchi akisema, “Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya tabianchi COP30, mjini Belém, itakuwa COP ya ukweli. Itakuwa wakati kwa viongozi wa dunia kuthibitisha umakini wa ahadi zao kwa sayari. Bila picha kamili ya Michango Inayohesabiwa Kila Taifa (NDCs), tunatembea tukifunga macho kuelekea uharibifu.”

Amehitimisha kwa kusema, “Tunahitaji viongozi wenye maono ya wazi, ambao wanaelewa kwamba mpangilio wa kimataifa si mchezo wa nambari sifuri. Karne ya 21 itakuwa na nguvu nyingi zaidi. Kwani ibaki katika amani, haiwezi kushindwa kuwa ya kimataifa.”