Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dunia ndani ya jengo moja la UN: Unachopaswa kufahamu kuhusu UNGA80

Mkutano wa kwanza wa kikao cha 80 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
UN Photo/Eskinder Debebe Mkutano wa kwanza wa kikao cha 80 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

Dunia ndani ya jengo moja la UN: Unachopaswa kufahamu kuhusu UNGA80

Masuala ya UM

Viongozi wa dunia wanakutana kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, kandoni mwa tawi la Mashariki la mto Hudson, eneo la Manhattan, kitongoji cha New York, kwa kile kinachotazamwa kuwa moja ya mikutano muhimu ya mwaka katika zama za karibuni.

Wawakilishi kutoka nchi zote 193 wanachama wa Umoja wa Mataifa – sambamba na wajumbe wa mataifa yenye hadhi ya uangalizi – watapata fursa kuzungumza kwenye Mjadala Mkuu, unaofanyika kwenye Ukumbi wa kipekee wa Baraza Kuu. Wakati huo huo, kwenye jengo la Makao Makuu, mlolongo wa mikutano ya ngazi ya juu itatatua changamoto kuu zinazokabili binadamu hivi sasa.

Majanga duniani yakiwa ni lukuki kuanzia vita hadi mabadiliko ya tabianchi, hadi ukosefu wa usawa wa kijinsia na sintofahamu kuhusu maadili yatokanayo na matumizi ya akili mnemba, Wiki Hii ni zaidi ya utamaduni. Ni wakati muhimu wa jamii ya kimataifa kutafakari, kuahidi upya na kutafakari upya mustakabali wa pamoja.

Matukio hayo yanaashiria kuanza kwa mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, (UNGA80), chombo kikuu cha maamuzi cha Umoja wa Mataifa. Mkutano wa mwaka huu unaenda sambamba na maadhimisho ya miaka 80 ya kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa.

Sasa nini cha kutarajia wakati wa UNGA80?

Annalena Baerbock (kushoto), Rais wa kikao cha 80 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa akifungua mkutano kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa.
UN Photo/Loey Felipe Annalena Baerbock (kushoto), Rais wa kikao cha 80 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa akifungua mkutano kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa.

Mjadala Mkuu: hotuba, hotuba na hotuba

Mjadala Mkuu ambao unaanza tarehe 23 mwezi Septemba, ndio jambo kubwa la Mkutano wa Baraza Kuu. Viongozi wa dunia watapanda kwenye mimbari mbele Ukumbi wa Baraza Kuu kuweka bayana vipaumbele vyao.

Muda wa hotuba wakati wa Mjadala huo Mkuu kwa wazungumzaji zaidi ya 193 ni dakika 15, lakini ni nadra kwao kuzingatai muda.

Utamaduni ni kwamba Brazil ndio ya kwanza kuhutubia ikifuatiwa na Marekani ambayo ni nchi mwenyeji.

Rais wa UNGA80 ni Annalena Baerbock, ambaye ni mwanamke 5 katika historia ya miaka 80 ya Umoja wa Mataifa kushika wadhifa huo. Yeye ataongoza mjadala wa mwaka huu ambao maudhui yake ni :‘Bora pamoja:miaka 80 na zaidi kwa ajili ya amani, maendeleo ya haki za binadamu.

Wakati gani nchi  yangu itazungumza?

Fahamu zaidi kuhusu mjadala mkuu.

Vita vimeangamiza Gaza kuigeuza vifusi.
© UNICEF/Mohammed Nateel Vita vimeangamiza Gaza kuigeuza vifusi.

Jawabu la mataifa mawili: ‘uko mbali zaidi kuliko wakati wowote’

Suluhisho la mataifa mawili, mfumo ulio pendekezwa wa kutatua mgogoro kati ya Israeli na Palestina ambao unalenga kuanzisha mataifa mawili kwa watu wa mataifa mawili, uko “mbali zaidi kuliko wakati wowote ule” kulingana na Katibu Mkuu wa UN alipozungumza Julai 2025.

Suluhisho la mataifa mawili lilianza kabla ya mgogoro wa sasa Gaza ulioanza Oktoba 2023 kufuatia mashambulizi ya kigaidi yaliyoanzishwa na wanamgambo wa kipalestina wa Hamas kusini mwa Israel na kuua watu wengi.

Wakati idadi ya watu waliouawa Gaza inakaribia 70,000 na mateka walioko mikononi mwa Israel bado wakiwa katika mateka katika eneo hilo, nchi wanachama wa UN wataendelea na mazungumzo juu ya jawabu la mataifa mawili katika mkutano wa kimataifa unaofanyika katika Makao Makuu ya UN Jumatatu tarehe 22 Septemba.

Mkutano huu ni mwendelezo wa mikutano iliyofanyika kwenye Baraza Kuu la UN Mkutano Mkuu wa UN Julai 2025, ambapo hakuna upande wa Israeli wala Marekani walioshiriki.

“Imekuwepo zaidi ya miongo saba tangu Baraza Kuu lilipoomba mara ya kwanza suluhisho la nchi mbili, Rais wa Baraza Kuu – 23 Mei 2025

Kufuatilia taarifa zote za UN hapa.

Kuadhimisha miaka 30 ya Tamko la Beijing: kuwawezesha wanawake na wasichana

Tamko la Beijing la mwaka 1995 na Mpango wa Utekelezaji, linachukuliwa kuwa ramani ya maendeleo ya hali ya juu zaidi ya kufanikisha usawa wa kijinsia na kuendeleza haki za wanawake na wasichana duniani kote.

Baada ya miongo mitatu tangu tamko hili la kihistoria, licha ya maendeleo kadhaa, UN Women, shirika mahsusi la UN linalojikita kwenye masuala ya wanawake, limesema kuna “ukinzani unaoongezeka dhidi ya haki za wanawake.”

Tarehe 22 Septemba, viongozi wa dunia watajadili Mpango wa Utekelezaji wa Beijing+30 unaolenga kufanikisha mambo yafuatayo kwa wanawake na wasichana wote: mapinduzi ya kidijitali, kujikwamua kutoka kwenye umaskini, ukosefu wa vurugu, uwezo kamili na usawa wa kufanya maamuzi, ushawishi sawa katika masuala ya amani na usalama pamoja na haki ya tabianchi.

Soma zaidi kuhusu usawa wa kijinsia katika ripoti ya Jinsia na SDGs

Tabianchi: Kukabiliana na joto

Dunia inapojitahidi kudhibiti kuongezeka kwa joto chini ya nyuzi joto 1.5 katika kipimo cha Selsiyasi kama ilivyokubaliwa kimataifa juu ya viwango vya kabla ya viwanda, mkutano utafanyika Jumatano 24 Septemba kuchambua kasi na kiwango cha hatari ya mzozo wa tabianchi duniani kote.

Viongozi wa dunia watawasilisha mipango mipya ya kitaifa ya hatua za tabianchi inayojulikana kama Mchango wa Kitaifa uliobainishwa au NDCs, ahadi za nchi kwa nchi zinazobainisha hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Mkutano pia utaalika viongozi kutoka serikali, sekta binafsi, na jamii ya kiraia, kuwasilisha mawazo ya kuendesha hatua katika kupunguza athari, kujiandaa, fedha na usahihi wa taarifa.

“Huu ni wakati wetu wa fursa,” amesema Mkuu wa UN, António Guterres.

Mkutano huu unafanyika kabla ya mkutano wa 30 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Mabadiliko ya tabianchi, COP30, ambao utaanza Brazil mwezi Novemba.

Soma zaidi hapa kuhusu UN na mabadiliko ya tabianchi

Roboti linaloweza kufanya kazi afanyazo binadamu likiwa kwenye moja ya maduka huko Kyoto nchini Japani.
© Unsplash/Lukas Roboti linaloweza kufanya kazi afanyazo binadamu likiwa kwenye moja ya maduka huko Kyoto nchini Japani.

Akili Bandia au Akili Unde: Kuweka Mipaka

Akili Bandia au AI imekuwa ikibadilisha dunia kwa kasi ikijumuisha vitu vyote kuanzia magari yanayojiendesha hadi uchambuzi wa picha za matibabu, kutoka usimamizi wa hesabu kwa biashara hadi algoriti za biashara ya fedha na kutoka wasaidizi wa kidijitali hadi tafsiri ya lugha kwa wakati halisi.

Hata hivyo, faida za AI hazisambazwi sawasawa, na nchi nyingi zinapata shida kupata zana zinazoweza kubadilisha jamii zao kwa kusaidia maendeleo na kuboresha maisha ya watu wa kawaida.

Kuenea kwake kwa haraka kunaleta hatari na changamoto nyingi, ikiwemo vitisho kwa usahihi wa taarifa na haki za binadamu, kama vile ufuatiliaji.

Kwa sasa, hakuna taasisi inayotambuliwa kusimamia AI kimataifa, hivyo viongozi wa dunia wanakusanyika New York tarehe 25 Septemba kujadili mfumo wa usimamizi wa AI unaojumuisha na kuwajibika.

“Bila mipaka ya kutosha, AI inaweza kuongeza zaidi ukosefu wa usawa na mgawanyiko wa kidijitali na kuathiri vibaya zaidi watu walioko katika hatari. Lazima tutumie fursa hii ya kihistoria … kwa manufaa ya ubinadamu wote,” amesema Mkuu wa UN.

Soma zaidi hapa kuhusu UN na AI

Mikutano mingine kadhaa inaendelea wakati wa wiki ya “ngazi ya juu.”