Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mradi wa IFAD wajengea uwezo wanawake Nepal ambao awali walighubikwa ukata

Bibha, mnufaika wa mradi wa IFAD, kutoka Nepal, akiwa amevaa sari ya bluu, amesimama katika mazingira ya kijijini.
© IFAD Mhusika mkuu wa mradi wa IFAD Bibha kutoka Nepal, ambaye mumewe alipoondoka Nepal kwenda Qatar kufanya kazi, Bibha alibakia nyumbani kulea sio tu watoto wao wawili bali pia wakwe zake.

Mradi wa IFAD wajengea uwezo wanawake Nepal ambao awali walighubikwa ukata

Ukuaji wa Kiuchumi

Nchini Nepal suala la waume kwenda kusaka ajira nje ya nchi na kuacha wake zao wakihaha kukimu familia zao katika mazingira ambamo wanawake wanakuwa hawana uthabiti wa kiuchumi limeanza kupatiwa muarobaoni.

Mhusika mkuu anayetumika kwenye hoja hiyo ni Bibha ambaye mumewe alipoondoka Nepal, taifa lililoko kusini-mashariki mwa Asia, kwenda Qatar kufanya kazi, Bibha alibakia nyumbani kulea sio tu watoto wao wawili bali pia wakwe zake.

Anasema “Awali hali ilikuwa mbaya. Sikufahamu kuhusu mapato na matumizi, na sikuwa na kipato.”

Mwanamke aliyevaa sari ya bluu na nyekundu akiendesha pampu ya maji nje ya nyumba ya vijijini huko Nepal.
© IFAD Mhusika mkuu wa mradi wa IFAD Bibha kutoka Nepal, ambaye mumewe alipoondoka Nepal kwenda Qatar kufanya kazi, Bibha alibakia nyumbani kulea sio tu watoto wao wawili bali pia wakwe zake.

Mkombozi ukawa Mradi wa pamoja wa Uwezeshaji Wanawake (JP-RWEE) unaotekelekezwa na Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya Kilimo, IFAD kwa kushirikiana na serikali.

Mradi ulimpata Bibha na wanawake wengine elimu ya fedha na biashara, anasema “Nilipokwenda Lahan kwa mafunzo, niliogofya kujitambulisha. Lakini taratibu nilifahamiana na wenzangu na kuanza kuelewa mafunzo.”

Sasa Bibha si tu mkufunzi wa wanawake wengine, bali anajua kutunza fedha na uhusiano na wakwe zake umeimarika na wana mipango ya kujenga nyumba pamoja.

“Sasa hivi familia inajadili na kupanga mipango pamoja na nyumbani kuna amani.”