LLDCs za Afrika zaibuka kiuchumi kutokana na kutumia vema jiografia ya maeneo yao - UNDP
LLDCs za Afrika zaibuka kiuchumi kutokana na kutumia vema jiografia ya maeneo yao - UNDP
Nchi za Afrika zisizo na bandari, (LLDCs), ambazo kwa muda mrefu zimechukuliwa kuwa na kasoro kijiografia, sasa zinaibuka kama uchumi wa kimkakati wa “kuunganishwa kwa ardhi,” badala ya kutengwa kwa kutokuwa na bahari.
Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo duniani, UNDP limesema mataifa hayo hivi sasa kwa kutumia nafasi yao ya kati kijiografia, kuimarisha miundombinu ya kikanda, na kukumbatia teknolojia za mabadiliko, yanageuka kuwa vichocheo muhimu vya biashara, uvumbuzi, na ujumuishaji wa bara.
UNDP imesema hayo Alhamisi Agosti 7 huko Azawa, Turkmenistan kunakofanyia mkutano wa tatu wa Umoja wa Mataifa wa LLDCs.
“Kutokaka na eneo la Biashara Huria la Afrika (AfCFTA) linalinaloendelea kukua kwa kasi, LLDCs sasa zinajipanga upya kama kitovu cha mabadiliko ya kijamii na kiuchumi barani Afrika,” amesema Dkt. Samuel Doe, Mwakilishi wa UNDP nchini Ethiopia, akizungumza na wanahabari huko Azawa, akiwakilisha UNDP Afrika.
Amenukuu nyaraka mpya ya msimamo iliyotolewa na UNDP iitwayo Uchumi wa Afrika Uliounganishwa na Bara: Njia za Mafanikio na Maendeleo, inayochunguza simulizi mpya kuhusu LLDCs barani Afrika.
Matumizi mema ya eneo la soko huru Afrika
Mathalani nyaraka inatoka maarifa ya kiutendaji na mifano hai inayoonesha jinsi AfCFTA na maendeleo ya kidijitali vinavyovunja vikwazo vya jadi vya kibiashara na kiuchumi—na kufungua fursa kubwa kwa biashara za kikanda na kimataifa.
Nyaraka hii inatoa muundo wa sera unaotekelezeka kwa ajili ya kuibuka kwa “Nchi za kiuchumi zisizo na bandari za baharini lakini zilizounganishwa Afrika ,” zikiziweka nchi hizi kama wachangiaji hai katika ukuaji endelevu na shirikishi wa bara.
Dkt. Doe ametaja ni kwa vipi nchi hizo za Afrika zinachangia kwenye uchumi wa Afrika kupitia malighafi na huduma.
Mathalani almasi kutoka Botswana, Lesotho na Zimbabwe. Shaba kutoka Zambia na Zimbabwe, Kahawa kutoka Uganda na Ethiopia bila kusahau Sukari kutoka Eswatini.
“Baadhi ya LLDCs kama Eswatini zimeunganishwa sana katika masoko ya kikanda, zikiwa na zaidi ya asilimia 88 ya mauzo ya nje yakienda katika nchi za Afrika. Vivyo hivyo, Rwanda, Lesotho, Malawi, Niger, Uganda na Zimbabwe zote zilikuwa na mauzo ya nje yaliyovuka asilimia 30 katika kipindi hicho, ikionyesha kiwango kikubwa cha ujumuishaji wa kikanda,” amesema Dkt. Doe.
Shirika la ndege la Ethiopia launganisha Afrika
Amemulika pia miundombinu ambayo ndio msingi muhimu kwa ajili ya kugeuza LLDCs za Afrika kuwa vituo vya uzalishaji na biashara kwa kuunganisha mataifa kwa njia ya bara au ardhi.
Mathalani reli ya Ethiopia hadi Djibouti imepunguza muda wa usafirishaji wa mizigo kutoka saa 72 hadi saa 12.
“Uganda, kwa kupitia uboreshaji wa reli ya kisasa, SGR, barabara ya kusafirisha vifaa kutoka Malaba–Kampala, inajipanga kuwa kitovu cha biashara ya ndani ya Afrika Mashariki, huku Ethiopia ikitumia shirika lake la ndege kama kiungo kikuu cha kimataifa kwa zaidi ya nchi 100 duniani,” amesema Mwakilishi huyo wa UNDP nchini Ethiopia.
‘Kuunganishwa na bara’ kunabadilisha simulizi: nchi zisizo na bandari sasa zinakuwa madaraja badala ya kuwa vizuizi. Kupitia AfCFTA, LLDCs zinaweza kubadili jiografia kuwa faida ya ushindani—kusafirisha bidhaa, huduma na data kwa kasi na gharama nafuu kote Afrika na nje ya bara,” ametamatisha Dkt. Doe.
Hatua hii ya UNDP inaendana na Mpango wa Awaza wa LLDCs (2024–2034), Ajenda 2063 ya Afrika, na Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs).
Soma ripoti nzima hapa.