Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wekeza kwenye unyonyeshaji mtoto maziwa ya mama, wekeza kwenye mustakabali wao

Mama akimnyonyesha mtoto wake nchini Tanzania.
UN News
Mama akimnyonyesha mtoto wake nchini Tanzania.

Wekeza kwenye unyonyeshaji mtoto maziwa ya mama, wekeza kwenye mustakabali wao

Afya

Wekeza kwenye unyonyeshaji mtoto maziwa ya mama, Wekeza kwenye mustakabali, ndio kauli mbiu ya Wiki ya unyonyeshaji duniani iliyoanza tarehe Mosi mwezi huu wa Agosti na itakunja jamvi tarehe 7. Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, WHO linapigia chepuo unyonyeshaji mtoto maziwa ya mama kutokana na faida zake.

Huko Dar Es Salaam, jiji kuu la Biashara la Taifa la Tanzania, lililoko Afrika Mashariki, video kutoka angani inatusogeza katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, kubwa hapa ni kumulika unyonyeshaji mtoto maziwa ya mama. 

Lakini kwanza unafahamu maana ya unyonyeshaji mtoto maziwa ya mama yake? Zarubia Kinyogo, ni Mtaalamu wa Lishe hapa hospitalini, anasema, Zarubia Kinyogo“Unyonyeshaji ni ulishaji wa mtoto mchanga au mtoto mdogo kupitia maziwa ya mama moja kwa moja kwenye chuchu ya mama. Lakini pia mama yule anaweza kukamua maziwa na kumpatia kwa kutumia aidha kikombe au chupa.”

Maziwa ya mama yana virutubisho vyote

Nikamuuliza faida za unyonyeshaji mtoto maziwa ya mama ni zipi? Kwanza kwa mtoto, anasema “Maziwa ya mama ni lishe bora. Tunasema lishe bora au lishe iliyokamilika kwa sababu ina virutubisho vyote. Ina wanga, ina protini na vitamini na madini. Kwa hiyo, tunasema kabisa ni mlo kamili unaojitosheleza."

Zarubia Kinyogo anaongeza kuw maziwa haya yana kinga yana kinga dhidi ya mtoto kwa yana Kumuepusha na maradhi mbalimbali ikiwemo kama uzio au aleji. Namaanisha mtoto na aleji ya mtoto na magonjwa ya pumu, magonjwa ya kisukari, magonjwa ya saratani na kadhalika. Lakini maziwa haya yana mmengenyo kwa urahisi. Mfumo mzima wa chakula kwa msukumo wa mtoto ni bado mchanga haujakomaa. 

Hivyo basi, maziwa haya yanamiminika kwa urahisi na kufyonzwa kwa urahisi na yanatumika kwa ufanisi kadiri mwili unavyohitaji. Lakini maziwa haya yapo tayari hayahitaji maandalizi ya aina yoyote. Kwa hiyo mama kumnyonyesha tu moja kwa moja bila hata matayarisho yaliyo mengi.

Mama akimnyonyesha mtoto wake nchini Tanzania.
UN News
Mama akimnyonyesha mtoto wake nchini Tanzania.

Mama akimnyonyesha mtoto maziwa husaidia kupunguza uzito wake

Zarubia anasema “Maziwa haya huwa yana rekebisha uzito wa mama. Inarekebisha uzito wa mama. Ule uzito mwingi wa uzazi unapungua na kupata uzito wake ulio kamili. Lakini maziwa haya kwa mama pia yanamsaidia kumuepusha na saratani. Saratani ya kizazi na hata saratani ya maziwa au matiti na pia husaidia kupunguza utokaji mwingi wa damu. Mama anapojifungua hutoka damu, kwa hivyo ile damu huwa inapungua kadri mama anaponyonyesha.”

Mtaalamu huyu wa lishe akaelezea mambo muhimu ambayo mama anapaswa kuzingatia punde tu anapojifungua, “Ndani ya ile saa moja baada ya kujifungua anatakiwa mtoto amuweke kwenye chuchu na aanze kuvuta yale maziwa iwe jambo la kwanza, lakini anamuhitaji yule mtoto anatakiwa na mama atumie mkono wake kushika makalio ya mtoto na yule mtoto na kichwa chake kikae kwenye kiwiko cha mkono ule, na amweke vizuri kwenye chuchu, na ile sehemu nyeusi ya chuchu, basi iweze kuingia vizuri katika mdomo wa mtoto ili aweze kufyonza vizuri.

Nyonyesha mtoto titi moja kwa dakika 20 au zaidi

Mama huyu anatakiwa ahakikishe kabisa mtoto anakaa katika ile ziwa moja la kuanzia dakika ishirini na kuendelea ili mtoto yule aweze kufyonza maziwa tunaita ya mbele ya kati na ya nyuma aweze kuyapata yote aweze kuyapata kupata virutubisho vyote vya kutosha. 

Lakini sambamba na hiyo, pia mama huyo anatakiwa asimpatie mtoto wake chakula cha aina yeyote wala kinywaji chochote hata kama ni maji. Mpaka atimize miezi sita natakiwa mpatie maziwa ya mama tu yanatosha kabisa.

Maziwa ya mama yana Omega3

“Yale makundi makuu matatu kwanza ya vyakula vya wanga, protini na mafuta yapo kwa kiasi kinachostahiki. Kwa hiyo ukuaji wa mtoto kimwili tunasema utakuwa vizuri kabisa. Lakini kuna ukuaji pia wa kiakili au ubongo. Na maendeleo mazuri ya ukuaji wa ubongo yanategemea kuna acids ambayo tunaita fatty acids au  Omega 3 fatty acids kitaalamu ambazo  ni nzuri katika ukuaji wa ubongo na ni aina hiyo ya mafuta tu hupatikana katika maziwa ya mama.”

Elimu ya unyonyeshaji watoto maziwa ya mama imeleta manufaa

“Baada ya kufika Muhimbili kitu ambacho nimejifunza ninashauri wamama wengine wakipate au Akiwapendelea kwa kufuatilia ni jinsi ya kunyoosha mtoto na jinsi ya kutenganisha muda kati ya kulisha muda flani na yeye katika hizi jamii zetu za kawaida kuna joto mtoto akiwa na njaa unamnyonyesha akilia unamnyonyesha Lakini baada ya kufika hapa tunaambiwa mtoto anatakiwa apewe maziwa kila baada ya masaa matatu. Kwa ukimpa maziwa kama ni saa tatu asubuhi tena mpaka saa sita saa sita mpaka saa tisa, Hivyo jinsi ya kurejesha kitu ambacho nilikuwa sijui wewe ni kuwa sijui kusikia.”

Ratiba ya kunyonyesha mtoto yapatia mama muda wa kujiandaa

“Faida kwa mtoto inamsaidia kupata ule muda wa kumeng’enya chakula tumboni na kwangu mimi pia inanisaidia kujiandaa kutoka muda ambao nampa maziwa kutoka saa tatu ili nijipange kama ni kutafuta maziwa kwenda kutafuta vitu vya kuongeza ili niweze kupata maziwa. Hivyo ili nikirudi saa sita apate maziwa ya kutosha. “